Na Mwandishi Wetu KAMISHNA Jenerali wa Uhamiaji Dk Anna Makakala, kuna umuhimu wa kuchukua hatua za dhati na za kimkakati ili kuhakikisha kuwa usawa wa kijinsia unakuwa sehemu ya maisha ya kila siku na kuhamasisha wanawake kujitokeza kushiriki katika nafasi za uongozi. Amesema kuna umuhimu wa kuendelea kuelimisha jamii kuhusu haki za kijinsia na umuhimu wa fursa sawa kwa wote ili kufikia usawa wa 50 kwa 50 kwa urahisi. Dk Makakala aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza kwenye siku ya jinsia ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), iliyofanyika jana chuoni hapo. Dk Makakala alisema kuna umuhimu wa kuhakikisha jamii inaondoa aina zote za ubaguzi wa kijinsia katika elimu, ajira, na uongozi na kuimarisha mifumo ya kisheria na kijamii ya kuzuia unyanyasaji wa kijinsia. Alisema kuna umuhimu wa kuhimiza wanaume kuwa sehemu ya suluhisho, kwa kushiriki katika mijadala na sera zinazohusu usawa wa kijinsia na kuwezesha wanawake kiuchumi, kuboresha upatikanaji wa fursa za ra...
Marato tv - Sauti ya Jamii