Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Biteko Ataka Wananchi Wapewe Majibu ya Huduma Kwa Haraka na Haki


📌 Aipongeza EWURA kwa taarifa yenye mchango muhimu kuimarisha sekta ya nishati

📌 Vyombo vya moto vinavyotumia gesi vyaongezeka kufikia 7,000

📌 Mahitaji ya umeme kufikia megawati 8,055 mwaka 2035

📌 Upatikanaji wa mafuta waendelea kuimarika nchini

📌 TANESCO yaendelea kuimarika na kupata faida


Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka watendaji wa sekta ya nishati kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi.

Pia, ameipongeza  Bodi ya Wakurugenzi na Wafanyakazi EWURA kwa uandaaji wa Taarifa za Maendeleo ya Sekta ya Nishati kwa Mwaka 2023/24 kwa kuwa  zina umuhimu mkubwa kwa Serikali katika kufanya maamuzi, kwani zinasaidia kuona mwenendo wa sekta ya nishati kwa  kuonesha  hali ya sekta hiyo  ya nishati, mafanikio, changamoto na fursa zilizopo katika kuiendeleza.

Dkt. Biteko ameeleza hayo leo Aprili 9, 2025 jijini Dodoma wakati aliposhiriki katika uzinduzi wa Taarifa za hizo Maendeleo ya Sekta ya Nishati kwa Mwaka 2023/24.

“ Wananchi wapewe majibu ya haraka na ya haki, taarifa hii imeonesha bado tuna kazi kubwa ya kufanya. Tunachotaka ni Watanzania kupata huduma iliyo bora na hiyo itasaidia kutokuwa na malalamiko ya upatikanaji wa huduma kutoka kwa wananchi,” amesema Dkt. Biteko.

Amesema kuwa Serikali inaendelea kujenga vyanzo vipya vya umeme na kuweka msukumo mkubwa katika uwekezaji wake ili kukabiliana na hatari ya uhaba wa umeme inayoweza kutokea zisipofanyika jitihada za makusudi na za haraka.

“Mahitaji ya umeme yameongezeka hadi megawati 254 ambapo ni sawa na kujenga mradi mwingine kama wa Kidatu, ifikapo mwaka 2030 mahitaji ya juu ya umeme yatakuwa megawati 4,878 na mwaka 2025 mahitaji ya juu ya umeme yatafikia megawati 8,055 taarifa hii inaonesha hatari kama hatutachukua hatua,” amebainisha Dkt. Biteko.

Kwa upande wa sekta ndogo ya gesi asilia, Dkt. Biteko amesema  kama zilivyo sekta nyingine za nishati kwa mujibu wa Taarifa hiyo, imeonesha kuwepo ongezeko la matumizi ya gesi asilia viwandani, majumbani na kwenye vyombo vya usafiri. Aidha, vituo vya kujaza gesi iliyoshindiliwa kwenye magari (CNG) vimeongezeka.

Kuhusu mafuta amesema  taarifa hiyo  inaonesha kuimarika kwa upatikanaji wa mafuta nchini pamoja na jitihada za kuhamasisha wawekezaji wa ndani kujenga vituo vya mafuta katika miji midogo na vijijini ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa bidhaa hiyo. Aidha, amezipongeza kampuni za mafuta kwa kushirikiana vizuri na Serikali.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesema pamoja na jitihada za Serikali kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika ya umeme, mafuta na gesi asilia bado sekta inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwepo mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu wa mazingira, upungufu na uchakavu wa miundombinu.

Ametaja changamoto zingine ni za rasilimali fedha kwa ajili ya uwekezaji na za maendeleo ya sayansi na teknolojia. Hata hivyo, ili kuondokana na changamoto hizo amesema , Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine, itaendelea kuhakikisha inaboresha, inaimarisha, inarahisisha na inawezesha upatikanaji wa nishati safi kwa Watanzania wote.

“ Namshukuru sana na kumpongeza Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa mchango mkubwa katika kuimarisha sekta ya nishati. Chini ya uongozi wake, tumeshuhudia maendeleo makubwa katika sekta hii ikiwemo ukamilishwaji wa miradi mikubwa ya kimkakati na kielelezo ambayo imeongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini, upatikanaji wa bidhaa za petroli, pamoja na ongezeko kubwa la matumizi ya gesi asilia hususani kwenye magari,” amesisitiza Dkt. Biteko. 

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati, Mhe. Judith Kapinga “Naendelea kumpongeza Rais Samia kwa kazi kubwa inayofanyika katika sekta ndogo ya nishati, na usimamizi mzuri wa Dkt. Biteko unaowezesha kupata mafanikio yote haya,” ameeleza Mhe. Kapinga.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi EWURA, Prof. Mark Mwandosya ameishukuru na kuipongeza Serikali kwa uwekezaji mkubwa inaoendelea kuufanya katika sekta ya nishati.

“ Hii miradi mikubwa hasa ya umeme mfano Bwala la Julius Nyerere inachukua muda mrefu hadi kukamilika kwake hivyo ni kiashiria kwamba tuanze sasa kutekeleza miradi mingine ili baada ya miaka kadhaa tusijekupata changamoto ya umeme,” amesema Prof. Mwandosya.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA), Dkt. James Andilile amesema kuwa uzinduzi wa taarifa hizo ni takwa la kisheria na tayari wameshafanya hivyo kwa upande wa sekta ya maji.

Amesema katika sekta ndogo ya umeme hadi kufikia Juni 2023/2024 uzalishaji wa umeme ulikuwa megawati 2,411 na sasa umefikia megawati 4,032.

“Kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme huduma imeimarika na sasa changamoto iliyokuwepo imeondolewa. Kuhusu gharama za bei ya umeme kutokana na uwekezaji katika miundombinu hali ya fedha TANESCO imeendelea kuimarika na mwaka wa tatu mfululizo imetengeneza faida kutokana na usimamizi wa Serikali wa kuondokana na mitambo ya kukodi ya kuzalisha umeme,” amesema Dkt. Andilile

Ameongeza kuwa katika sekta ya mafuta hadi kuishia Juni 2023/2024 vituo vya mafuta vilikuwa 2,361 sawa na ongezeko la asilimia 10, kukiwa na vituo 480 vijijini sawa na ongezeko la asilimia 12. Pia, kuhusu gesi asilia amesema  katika mwaka 2020/2023 vyombo vya moto vilivyokuwa vinatumia gesi asilia vilikuwa 7,000  na kufikia Machi mwaka huu vimefikia 15,000 ikiwa ni sawa na asilimia 49.








Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

Wananchi Serengeti Wamtaja Dkt Rhimo Nyansaho Kama Chachu ya Maendeleo Kwao

Na Shomari Binda-GMTV  WANANCHI Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemtaja Dkt.Rhimo Nyansaho kama chachu ya maendeleo kupitia taasisi yake ya Nyansaho Foundation. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na GMTV wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu mchango wake umeonekana katika kuisaidia jamii. Wamesema ukifika Jimbo la Serengeti kila Kata na Kijiji huwezi kukosa mkono wa Dkt.Nyansaho kuchangia na kusaidia jamii kuanzia elimu,afya,maji na masuala mengine ya jamii. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mwita Sagati amesema wapo watu wanaojitokeza kusaidia jamii kipindi cha uchaguzi kwa kulenga kupata uongozi lakini imekuwa tofauti kwa Dkt.Nyansaho. Sagati amesema iwapo atajitokeza kuomba nafasi ya ubunge wapo tayari kumpambania na kumchagua ili aweze kuendelea kutoa mchango wake katika kusaidia jamii. " Tunashukuru sana mchango wa Dkt.Nyansaho kwa kuchangia shughuli za maendeleo hapa Serengeti. " Wengine huwa wanakuja nyakati za uchaguzi lakini huyu mchango wake ni ...

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...