Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Rais Samia Atembelea Makumbusho ya Muasisi wa Taifa la Angola,Apolelewa Kijeshi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitembelea Makumbusho ya Rais wa kwanza na Muasisi wa Taifa la Angola, Hayati António Agostinho Neto katika eneo la Public Square Jijini Luanda, tarehe 08 Aprili, 2025. Rais Dkt. Samia  amepokelewa kwa heshima ya kijeshi katika eneo hilo la Makumbusho  na kisha kuweka  shada la maua katika Mnara wa Kumbukumbu wa Rais wa kwanza na Muasisi wa Taifa hilo Hayati António Agostinho Neto.

Waziri Mkuu Ashiriki Kikao Cha Bunge

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Aprili 8, 2025 ameshiriki Kikao cha Kwanza cha  Mkutano wa Kumi na Tisa wa Bunge  jijini Dodoma.

Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua ataka Vikwazo dhidi ya Rais William Ruto

 Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, amezitaka jamii za kimataifa kuwekea vikwazo Rais wa Kenya William Ruto kwa tuhuma za kuchochea mizozo nchini Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ili kulinda maslahi yake ya kibiashara. Akizungumza katika mahojiano na kituo cha televisheni cha KTN usiku wa kuamkia leo, Gachagua alidai kuwa Rais Ruto anashirikiana na wanamgambo wa RSF wa Sudan, Mohammed Hamdan Dagalo (Hemedti), pamoja na viongozi wa kundi la waasi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda, kwa lengo la kulinda mtandao wa biashara ya dhahabu. “Nataka kuomba jamii ya kimataifa wazingatie hali hii nchini kwetu. Hatutapata amani wala usalama katika eneo hili endapo hatutamdhibiti Rais William Ruto, ambaye amejaa ubinafsi na tamaa ya kujinufaisha kibiashara katika kanda hii,” alisema Gachagua. Aliongeza, “Kwa vifo vinavyotokea Sudan, kamanda halisi wa RSF si Hemedti, bali ni William Ruto, kwa sababu ili harakati yoyote ifanikiwe, inahitaji rasilimali. Pesa za dhahabu...

Mbunge Ghati Chomete Awaombea Maji Wananchi wa Kata za Bisumwa,Nyankanga na Bukabwa Wilaya ya Butiama

Na Shomari Binda-Musoma  MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Mara Ghati Chomete amewaombea upatikanaji wa maji wananchi wa Kata za Bisumwa,Nyankanga na Bukabwa zilizopo Wilaya ya Butiama. Maombi ya mbunge huyo ameyatoa leo April 8 bungeni katika kikao cha kwanza cha mkutano wa 19 wa bunge la bajeti alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kwenye Wizara ya Maji. Kabla ya kuuliza swali hilo mbunge huyo ameishukuru serikali kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maji ili kuwezesha wananchi kupata maji kwenye maeneo yao. Amesema miradi hiyo imewezesha kumtua mama ndoo kichwani na kumshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwaajili ya miradi hiyo. " Mheshimiwa Naibu Spika nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza kwenye Wizara ya Maji. " Kwanza naidhukuru serikali kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji kwa mkoa wa Mara,swali langu ni lini wananchi wa Kata za Bisumwa,Nyankanga na Bukabwa wilayani Butiama watafikishiwa huduma ya maji?",ameuliza Akiji...

Happy Birthday George Marato

GMTV inakutakia George Marato, heri njema na baraka tele katika siku yako ya kuzaliwa! Hongera kwa kufikia hatua nyingine ya maisha. Uendelee kuwa na afya njema, furaha, na mafanikio katika kila unachofanya. Siku hii iwe ya kipekee kwako, ikujaze matumaini mapya na kumbukumbu nzuri zisizosahaulika.

Balozi Dkt Nchimbi Akutana wa Askofu wa Jimbo la Mbinga

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akizungumza jambo na Askofu John Chrisostom Ndimbo wa Jimbo Katoliki la Mbinga, walipokutana Uwanja wa Ndege wa Songea, mkoani Ruvuma, Jumatatu tarehe 7 Aprili 2025.