Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu kuongoza harambee ya Mei Mosi Kitaifa

  WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa usiku wa leo Aprili 5, 2025 anaongoza harambee ya kuwezesha maadhimisho ya Mei Mosi Kitaifa kwenye ukumbi wa Royal Village jijini Dodoma.  Maadhimisho hayo yatafanyika Kitaifa mkoani Singida Mei 01, 2025 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ridhiwani Kikwete, Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamuhokya, Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Martha Mlata ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria harambee hiyo.

MISA Tanzania yaipongeza TEF Kwa kufanya uchaguzi salama.

Mwandishi wetu Dodoma Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika, Tawi la Tanzania ( MISA Tan) Bwana Edwin Soko amelipongeza jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Kwa kufanya uchaguzi wao salama na kuwapata viongozi wake watakaokuwa na dhamana ya kuingiza TEF Kwa miaka minne . MISA Tan tunampongeza Mwenyekiti Deodatusi Balile na kamati yake ya utendaji Kwa kuchaguliwa tena kuiongoza TEF, hiyo ni imani kubwa Kwa wana TEF" alisema Edwin Soko Mwenyekiti wa MISA Tan. Bwana Soko pia aliongeza kuwa, MISA Tan ina mahusiano mazuri na TEF hivyo itaendelea kufanya kazi Kwa ukaribu na TEF.

Mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere wakamilika rasmi - Dkt Biteko

  📌 Asema ni ndoto ya watanzania kupata umeme wa uhakika    📌 Asisitiza kazi iliyobaki ni kuimarisha miundombinu ya kuwafikishia wananchi umeme   📌 Rais Samia na Rais wa Misri kuzindua rasmi Mradi wa Julius Nyerere Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Watanzania kutegemea kupata umeme wa uhakika baada ya Mradi wa kufua umeme kutoka Bwawa la Julius Nyerere uliokuwa ukisubiriwa kwa shauku kubwa na Watanzania  kukamilika  rasmi.  Dkt. Biteko ameyasema hayo April 5, 2025 baada ya kutembelea Mradi huo akiwa ameambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na uwekezaji, Mhe. Profesa Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Hamadi Masauni pamoja na Viongozi wengine mbalimbali. Amesema hivi sasa mitambo yote tisa imekamilika na inafanya kazi tayari, amefafanua kuwa kukamilika kwa Mradi huo kumechangiwa na maono ya Rais wa Awamu ya Sita, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye aliupo...

Mwenyekiti wa Wazazi Butiama anogesha maadhimisho ya Jumuiya ya Wazazi

  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Wilaya ya Butiama, ndugu Baraka Imanyi(OBAMA) ameshiriki katika maadhimisho ya Wiki ya WAZAZI Kwenye Kata Ya Nyakanga na Kata Ya Bisumwa yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Mkiringo, Kata ya Nyankanga na Shule ya Msingi Kaginakeru, Kata ya Bisumwa wilayani Butiama. Katika maadhimisho hayo ambayo yamefanyika Aprili 4 mwaka huu 2025,amewata wazazi kusimamia mmonyoko mkubwa maadili ya watoto wao kwani amesema ni jukumu la jumuiya hiyo katika kuwezesha malezi katika familia. Amesema taifa limajengwa na watu wenye maadili mema na kwamba wazazi wasikwepe jukumu hilo na kuitwusha serikali mzigo huo. "Sisi kama wazazi ni jukumu letu kusimamia maadili ili kulinda Taifa letu,hatuwezi kulalamikia vitendo vya rushwa,ukatili na unyanyasaji katika jamii yetu wakati tukijua mambo haya yanafanywa na watoto wetu,tukisimamia malezi na maadili tutakuwa tumelisaidia Taifa na kumsaidia Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kuongoza watu wema"akisema Obama...

Rais Samia aandika historia kwa kufungua Makao Makuu ya Mahakama Tanzania

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania, Tume ya Utumishi wa Mahakama pamoja na Nyumba za Makazi ya Majaji Mkoani Dodoma, tarehe 05 Aprili, 2025.

Rais Mwinyi kuelekea Uingereza kushiriki mkutano wa CTIS

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe, Dkt.Hussein Ali Mwinyi ataondoka nchini leo kuelekea Jijini London, nchini Uingereza kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe 6 hadi 9 Aprili 2025 kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano wa Biashara na Uwekezaji wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Trade & Investment Summit 2025). Katika ziara hiyo Rais Dkt.Mwinyi matukio mengine atakayoshiriki ni kukutana na Viongozi waandamizi wa Serikali ya Uingereza na Taasisi zake, atakutana na  Diaspora wa Tanzania waliopo nchini Uingereza, atakutana na Sir Tony Blair , Waziri Mkuu Mstaafu na Kiongozi wa Tony Blair Institute (TBI), pia atakutana na wadau wa uwekezaji katika uchumi wa bluu. Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi atakutana na wadau wa  uwekezaji katika sekta ya utalii, filamu, viwanda, nishati ikiwemo pia mafuta na gesi. Vilevile Rais Dkt.Mwinyi atashuhudia kusainiwa kwa makubaliano ya ushirikiano baina ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Chuo Kikuu cha Kent kwa ajili ya utafiti wa k...