Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Wilaya ya Butiama, ndugu Baraka Imanyi(OBAMA) ameshiriki katika maadhimisho ya Wiki ya WAZAZI Kwenye Kata Ya Nyakanga na Kata Ya Bisumwa yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Mkiringo, Kata ya Nyankanga na Shule ya Msingi Kaginakeru, Kata ya Bisumwa wilayani Butiama.
Katika maadhimisho hayo ambayo yamefanyika Aprili 4 mwaka huu 2025,amewata wazazi kusimamia mmonyoko mkubwa maadili ya watoto wao kwani amesema ni jukumu la jumuiya hiyo katika kuwezesha malezi katika familia.
Amesema taifa limajengwa na watu wenye maadili mema na kwamba wazazi wasikwepe jukumu hilo na kuitwusha serikali mzigo huo.
"Sisi kama wazazi ni jukumu letu kusimamia maadili ili kulinda Taifa letu,hatuwezi kulalamikia vitendo vya rushwa,ukatili na unyanyasaji katika jamii yetu wakati tukijua mambo haya yanafanywa na watoto wetu,tukisimamia malezi na maadili tutakuwa tumelisaidia Taifa na kumsaidia Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kuongoza watu wema"akisema Obama huku akishangiliwa.
Mwenyekiti huyo wa wazazi wilaya ya Bitima katika ziara hiyo amepata fursa ya kupanda miti pamoja na wana chama Wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya ya WAZAZI katika Kata hizo.
Katika hatua nyingine kiongozi huyo amejadili na walimu kuhusu maendeleo ya shule pamoja na kutatua baadhi ya kero zilizopo katika shule hizo.
Katika Ujenzi Wa Jumuiya Na Chama Jumuiya Ya Wazazi Wilaya Ya BUTIAMA Chini Ya Mwenyekiti wake ndugu Baraka Imanyi (OBAMA) Imekuwa Ikijikita Sana Kwenye Utatuzi Wa Changamoto Kwenye ngazi ya Jamii
Bw Obama amechangia mifuko 10 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika shule ya msingi Kaginakeru, huku akichangia fedha Kwaajili Ya Kuhakikisha Wanafunzi Wanapata Lishe Bora Ya Chakula katika shuke ya Mkiringo.