-Achangisha milioni 45.6 KMT Mangucha, SDA Nyabitoche NA MWANDISHI WETU, Tarime Mfanyabiashara maarufu nchini na mkazi wa Tarime Nyambari Nyangwine ameendesha harambee katika Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT) lililopo kijiji cha Mangucha katika kata ya Nyanungu wilayani Tarime na kufanikisha kupatikana kwa shilingi zaidi ya milioni 27. Katika harambee hiyo iliyofanyika kanisani hapo machi 9 mwaka 2025, Nyambari ambaye amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Tarime amechangia shilingi milioni 10,huku akisindikizwa na rafiki zake, wakiwemo madiwani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Vijijini Diwani wa Kata ya Nyanungu, Tiboche Richard alishiriki katika harambee hiyo ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo. Aidha Nyambari aliahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 12 kwa ajili ya kuchangia makanisa mbalimbali yaliyopo katika kata hiyo kwa lengo la kutaka nyumba hizo za Mungu zitumike kuleta mabadiliko hasa katika kusimamia amani kws maelezo ndio msingi wa Maendeleo. “Mimi ni mzaliwa wa kata hii, n...