Na Shomari Binda-Musoma
KASI ya ujenzi wa shule mpya za sekondari katika jimbo la Musoma Vijijini umezidi kushika kasi kubwa ili kuongeza idadi ya shule na kutoa fursa ya ukaribu wanafunzi kupata elimu.
Kufuatia hilo wananchi wa Kata ya Etaro Kijiji cha Mmahare wameanza ujenzi wa msingi wa madarasa ya shule mpya ya sekondari ikiwa shule ya tatu kwenye Kata hiyo.
Leo machi 10/ 2025 mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo amekabidhi kamati ya ujenzi wa shule hiyo mifuko 50 ya saruji kati ya mifuko 155 aliyoahidi kuendelea na ujenzi na watakabidhiwa mingine kadri wanavyotumia.
Hivi karibuni mbunge wa jimbo aligawa saruji mifuko 150 kwa kila kijiji kinachojenga sekondari mpya fedha za saruji hiyo ni zile za mfuko wa jimbo
Profesa Muhongo wakati akikabidhi mifuko ya saruji Kijiji cha Mmahare Kata ya Etaro amekipongeza na kukipa hongera kwa kasi nzuri ya ujenzi na tayari kimetumia mifuko yote 150.
" Nipongeze kasi kubwa ambayo inafanywa na wananchi wa Kijiji cha Mmahare Kata ya Etaro kwenye ujenzi wa shule mpya ya tatu ya sekondari.
"Leo machi 10 nimeikabidhi kamati ya ujenzi mifuko 50 ya saruji ili kuendelea na hatua ya ujenzi na wataendelea kupokea mifuko mingine kadri wanavyotumia",amesema.
Kwenye miradi yote ya ujenzi wa shule mbunge huyo huwa anaendesha harambee kuchangia ujenzi unaofanywa kwa kutumia nguvukazi na michango ya fedha za mfuko wa jimbo
Mbunge Muhongo ameendelea kuwaomba wadau mbalimbali wa elimu kuchangia maendeleo ya elimu jimboni humo.



Comments
Post a Comment