-Achangisha milioni 45.6 KMT Mangucha, SDA Nyabitoche
NA MWANDISHI WETU, Tarime
Mfanyabiashara maarufu nchini na mkazi wa Tarime Nyambari Nyangwine ameendesha harambee katika Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT) lililopo kijiji cha Mangucha katika kata ya Nyanungu wilayani Tarime na kufanikisha kupatikana kwa shilingi zaidi ya milioni 27.
Katika harambee hiyo iliyofanyika kanisani hapo machi 9 mwaka 2025, Nyambari ambaye amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Tarime amechangia shilingi milioni 10,huku akisindikizwa na rafiki zake, wakiwemo madiwani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Vijijini
Diwani wa Kata ya Nyanungu, Tiboche Richard alishiriki katika harambee hiyo ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo.
Aidha Nyambari aliahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 12 kwa ajili ya kuchangia makanisa mbalimbali yaliyopo katika kata hiyo kwa lengo la kutaka nyumba hizo za Mungu zitumike kuleta mabadiliko hasa katika kusimamia amani kws maelezo ndio msingi wa Maendeleo.
“Mimi ni mzaliwa wa kata hii, nitachangia maendeleo ya makanisa mengine manne, kila kanisa nitalichangia shilingi milioni tatu,” Nyambari ambaye pia ni mfanyabiasha, mwandishi na mchapishaji wa vitabu maarufu nchini Tanzania, aliwambia waumuni wa kanisa hilo na kuibua shangwe na vigelegele.
Makanisa yatakayonufaika na mchango huo ni Romani Katoliki, Anglikana, KKKT na SDA.
Katika hotuba yake kwenye harambee hiyo, Nyambari aliwahimiza wananchi wa wilaya ya Tarime kuwa na upendo na kuendelea kudumisha amani kwa kuwachukia watu wanataka kuwagawa kwa misingi yoyote ya kidini koo ama kabila.
Kwa sababu hiyo Nyambari aliwataka wananchi wa kata hiyo na wilaya kwa ujumla kuwekeza katika elimu na kulipa kipaumbele suala la elimu ya ujasiriamali kwa vijana wao.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Askofu wa KMT Dayosisi ya Tarime, Albert Jera Randa na Askofu Amos Joseph Muhagachi wa KMT Dayosisi ya Shirati.
Harambee hiyo ilifanyika siku moja baada ya Nyambari kuendesha harambee nyingine katika Kanisa la SDA Nyabitocho na kufanikisha kupatikana kwa shilingi milioni 18.6, ambapo yeye mwenyewe alichangia shilingi zaidi ya milioni 10.
Akiwa katika changisho la Nyabitocho SDA, Nyambari pia alitangaza kuchangia shilingi milioni mbili katika kanisa jirani la SDA Kyoruba Mlimani.
Siku hiyo hiyo, Nyambari alifika katika Kanisa la EAGT Sirari na kuichangia kwaya ya kanisa hilo shilingi milioni mbili.
Hata hivyo Nyambari amesema yeye kama mwana Tarime yupo tayari wakati wowote kutoa msaada kwa taasisi yoyote ya kijamii,dini na watu wenye malengo ya kuharakisha Maendeleo ya wilaya ya Tarime.


.jpg)


Comments
Post a Comment