Na Shomari Binda-Musoma DIWANI wa Kata ya Makoko na Meya wa manispaa ya Musoma Patrick Gumbo ametoa fursa ya vijana wa Kata hiyo kupata mkopo wa pikipiki kwa kutoa kianzio cha laki 2 Fursa hiyo ameitangaza jana februari 3 kwenye Mkutano Mkuu wa Kata wakati mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo akielezea utekelezaji wa ilani. Amesema ipo fursa hiyo iliyotolewa na mbunge kwa vijana wa jimbo la Musoma mjini kupata mkopo wa pikipiki kwa kutanguliza laki 3 na kulipa kidogo kidogo kwa kipindi cha mwaka mzima kutoka moja ya taasisi za kifedha ambapo tayari wapo waliopata mikopo hiyo. Gumbo amesema kwa kuiona fursa na kutaka pia vijana wa Kata yake wanapata wengi zaidi ametangaza kila kijana atakayetoa laki 2 yeye ataongezea laki 1 na kupata pikipiki. Amesema wasisikilize maneno ya pembeni kwamba kuna watu wanapendelewa kupewa pikipiki jambo ambalo sio kweli bali upo utaratibu wa kupata mkopo nafuu ambao mbunge ana usimamia. " Ambaye yupo tayari atoe laki 2 mimi ntamuong...
Marato tv - Sauti ya Jamii