Na Shomari Binda-Musoma
DIWANI wa Kata ya Makoko na Meya wa manispaa ya Musoma Patrick Gumbo ametoa fursa ya vijana wa Kata hiyo kupata mkopo wa pikipiki kwa kutoa kianzio cha laki 2
Fursa hiyo ameitangaza jana februari 3 kwenye Mkutano Mkuu wa Kata wakati mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo akielezea utekelezaji wa ilani.
Amesema ipo fursa hiyo iliyotolewa na mbunge kwa vijana wa jimbo la Musoma mjini kupata mkopo wa pikipiki kwa kutanguliza laki 3 na kulipa kidogo kidogo kwa kipindi cha mwaka mzima kutoka moja ya taasisi za kifedha ambapo tayari wapo waliopata mikopo hiyo.
Gumbo amesema kwa kuiona fursa na kutaka pia vijana wa Kata yake wanapata wengi zaidi ametangaza kila kijana atakayetoa laki 2 yeye ataongezea laki 1 na kupata pikipiki.
Amesema wasisikilize maneno ya pembeni kwamba kuna watu wanapendelewa kupewa pikipiki jambo ambalo sio kweli bali upo utaratibu wa kupata mkopo nafuu ambao mbunge ana usimamia.
" Ambaye yupo tayari atoe laki 2 mimi ntamuongezea laki 1 na mbunge ataongeza laki 1 unapata pikipiki na " offer" hii natangaza kwa watu 20 wa kwanza ntaandaa milioni 2.
" Licha ya hili la pikipiki kuna suala la ofisi yetu ya chama ya Kata nimeshatoa milioni 2 kwaajili ya kuchangia ujenzi wake na leo mbunge yupo naamini atatuchangia",amesema.
Akizungumza na wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM Kata ya Makoko mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amesema anashukuru viongozi wa Kata hiyo kukubali namna utekelezaji wa ilani ulivyofanikiwa kwa kufikiwa na miradi mbalimbali.
Amesema kazi yake ni kufatilia na kupatikana kwa miradi hiyo na Rais Dkt.Ssmia Suluhu Hassan anatoa fedha nyingi kwa utekelezaji wake.
Kuhusiana na ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Makoko ameahidi kuchangia milioni 3 ili viongozi wapate eneo lao la kuendesha shughuli za chama.
Mbunge huyo atakamilisha ziara yake ya kutembelea Kata kwa Kata kuelezea utekelezaji wa ilani hapo kesho februari 5 kwa kuitembelea Kata ya Mshikamano.


.jpg)
Comments
Post a Comment