Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini amewataka vijana kuendelea kumuamini ili azidi kuwafungulia milango ya fursa ambayo itapelekea kupata ajira na kujiimarisha kiuchumi.
Akizungumza katika Kikao cha Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Butiama kilichofanyika katika Ukumbi wa Kanisa la Romani Katoliki Nyamisisye Kata ya Kukirango, Wilaya ya Butiama mkoani Mara leo Februari 3, 2025 Mhe. Sagini amesema kuwa tangu alipochaguliwa kuwa mbunge amekuwa akishirikiana na vijana kutatatua changamoto zao.
"Vijana wa Butiama ni mashuhuda tosha kuwa sijawahi kuwa juu na mara zote jambo lao huwa ni langu ndio maana tumefanikiwa kuwafungulia fursa kupitia matamasha mbalimbali pia na miradi inayoendelea ndani na nje ya Jimbo la Butiama," amesema Mhe. Sagini
Akizungumza awali Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Butiama Ndg. Mathayo Kitenyi amempongeza Mbunge Sagini kwa kuwajali kwani ni mara ya pili amekuwa akifika katika Kikao cha Baraza hilo na kubeba changamoto na kwenda kuzifanyia kazi ambapo matokeo chanya yameonekana.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Butiama Ndg. Christopher Siagi amesema kuwa hicho anachokifanya Mbunge Sagini ni utekelezaji wa Ilani ya Chama chini ya Mwenyekiti CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan hivyo kutokana na kazi kubwa iliyofanyika kuna kila sababu ya kuwaomba wananchi ridhaa ya kuwatumikia tena katika uchaguzi ujao.




.jpg)







Comments
Post a Comment