Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Shilingi Trilioni 8.2 Zatumika Kukopesha Wanafunzi Katika Kipindi Cha Miaka 20-majaliwa.

_▪️Asema Serikali ilifuta tozo za kulinda thamani ya fedha ili kuondoa changamoto katika urejeshaji wa mikopo._ WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imetumia shilingi trilioni 8.2 kugharamia wanafunzi tangu ilipoanzishwa. Amesema kuwa pia katika kipindi hicho wanafunzi takribani 830,000 wamenufaika na mfumo huo wa ugharimiaji wa elimu ya juu kupitia Bodi ya mikopo. Amesema hayo leo Jumatatu (Februari 17, 2025) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, iliyofanyika kwenye Kituo cha Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. “Mafanikio tuliyonayo leo, ni matokeo ya utashi wa kisiasa, uongozi thabiti, maono na michango ya viongozi wetu. Viongozi wetu katika awamu zote walifanya kazi kubwa ya kuhakikisha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inafanya vizuri, viongozi wetu walioona mbali kuanzisha mfumo huu wa ugha...

Wanu H. Ameir Atoa Zawadi Kwa Wanafunzi Waliopata Division One

Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) chini Mwenyekiti wake, Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb) tarehe 16 Februari, 2025 iliandaa Mahafali ya Tatu (3) ya kuwapongeza Wanafunzi waliofaulu kidato cha Nne (4) wa Skuli ya Hasnuu Makame ambao walipata Division 1 kwa wanafunzi 51 na Division 2 kwa mwanafunzi 1. Mgeni rasmi wa Hafla katika Mahafali ya Tatu ya Skuli ya Hasnuu Makame alikuwa ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb) Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb) Alitoa zawadi maalumu kwa wanafunzi waliopata ufaulu wa juu wa division 1 ya point 7, 8 na 9, na kwa wanafunzi wengine walipatiwa zawadi za mabegi, vifaa vya shule, pamoja na pesa. Katika Hotuba yake, Mwenyekiti na Mwanzilishi wa MIF, Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb) amesema amefurahishwa sana na jitihada zilizofanywa na wanafunzi hao, na ahadi walioitekeleza ambayo waliitoa mwaka jana.  Mhe. Wanu Hafidh Ameir ameahidi kujenga dahalia (darasa) nyengine ili Skuli iweze kuchukua wanafun...

Uvuvi Wa Vizimba Unatazamiwa Kuinua Uchumi Mkubwa Wa Musoma Vijijini

Na Shomari Binda-Musoma  UVUVI wa samaki kupitia njia ya vizimba umedaiwa kuwa moja ya njia ya kuinua uchumi mkubwa wa wananchi wa jimbo la Musoma vijijini. Hayo yamesemwa na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo leo februari 17 2025 baada ya kuelezwa na wavuvi hao namna wanavyonufaika na uvuvi huo. Muhongo amesema wavuvi kwa kuendelea kuzingatia maelekezo ya wataalam na maafisa uvuvi wanakwenda kuondokana na umasikini. Amesema ziwa Victoria lina umri wa takribani miaka 400,000 na ujazo wake wa kawaida ni kilomita za ujazo 2,760 (2,760 cubic kilometres).  Ameekeza kuwa mvua za mwaka jana ziliongeza ujazo wa maji ndani ya bonde la Ziwa Victoria lenye ukubwa kilomita za mraba 195,000 (195,000 square kilometres)lilikuwa na ongezeko la kina cha takribani mita 1.7 (ca. 1.7 meters depth) Mbunge huyo amesema Kata 18 kati ya Kata 21 za jimbo zina ufukwe wa Ziwa Victoria kwa hiyo asilimia 85.7 (85.7%) za Kata  zina fursa nzuri za kutumia raslimali za maji ya ...

Kamati ya Waziri Jafo wageni Kariakoo yaendelea kuhoji wafanyabiashara

Na Mwandishi Wetu KAMATI iliyoundwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Selemani Jafo kuchunguza wafanyabiashara wa kigeni maeneo ya Kariakoo imefikia asilimia 50 ya uchunguzi wake na imeahidi kukabidhi ripoti hiyo Machi 2 kama ilivyoagizwa. Februari 2 Waziri Jafo aliunda Kamati ya watu 15 kuchunguza wafanyabiashara wa kigeni eneo la Kariakoo inayoongozwa na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Profesa Edda Lwoga Aliunda Kamati hiyo baada ya agizo la Rais Samia alitoa agizo hilo Januari 30, 2025, Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa halfa ya chakula cha mchana alichokiandaa kwa ajili ya washiriki wa shughuli ya uokoaji wa kuporomoka kwa jengo Kariakoo. Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Edda Lwoga ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE). Alisema baada tu ya uteuzi walianza rasmi kazi ya kuwahoji wafanyabiashara wa makundi mbalimbali kama machinga, wauza vifaa vya umeme, vifaa vya magari,  vipodozi na biashara zi...

Majaliwa Amwakilisha Rais Dkt. Samia Kwenye Kilele Cha Maadhimisho Ya Miaka Ishirini Ya Heslb

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Februari 17, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, inayofanyika kwenye Kituo cha Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yaliambatana na kliniki za huduma katika mikoa 7 nchini yakilenga kutoa elimu kwa wadau muhimu wa masuala ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu. kaulimbiu ya maadhimisho ni _”Maadhimisho ya miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu- Athari chanya, Ubunifu na Huduma’’._

Dkt. Biteko Awahimiza Watanzania Kuliombea Taifa

📌 *Asema amani ya nchi ilindwe kwa wivu mkubwa* 📌*Asisitiza uchaguzi Mkuu wa Oktoba usiligawe Taifa* 📌*Asema Watanzania waendelee kumuombea Rais Samia kwa kazi nzuri anazofanya* 📌 *Serikali kuboresha mipango yake kulingana na mahitaji ya dunia* *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuiombea nchi pamoja na Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. “ Tuendelee kuliombea kanisa, tuendelee kuiombea nchi yetu na Rais wetu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambae kwa kweli anafanya kazi nzuri na sisi tunaofanya kazi karibu naye tunaona,” amesema Dkt. Biteko. Dkt. Biteko amesema hayo leo Februari 16, 2025 wakati akishiriki ibada katika Kanisa la Africa Inland Church Chang’ombe jijini Dar es salaam. Amewahimiza Watanzania kudumisha upendo na amani nyakati zote hususan kipindi hiki kuelekea Uchaguzi...