Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) chini Mwenyekiti wake, Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb) tarehe 16 Februari, 2025 iliandaa Mahafali ya Tatu (3) ya kuwapongeza Wanafunzi waliofaulu kidato cha Nne (4) wa Skuli ya Hasnuu Makame ambao walipata Division 1 kwa wanafunzi 51 na Division 2 kwa mwanafunzi 1.
Mgeni rasmi wa Hafla katika Mahafali ya Tatu ya Skuli ya Hasnuu Makame alikuwa ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb)
Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb) Alitoa zawadi maalumu kwa wanafunzi waliopata ufaulu wa juu wa division 1 ya point 7, 8 na 9, na kwa wanafunzi wengine walipatiwa zawadi za mabegi, vifaa vya shule, pamoja na pesa.
Katika Hotuba yake, Mwenyekiti na Mwanzilishi wa MIF, Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb) amesema amefurahishwa sana na jitihada zilizofanywa na wanafunzi hao, na ahadi walioitekeleza ambayo waliitoa mwaka jana.
Mhe. Wanu Hafidh Ameir ameahidi kujenga dahalia (darasa) nyengine ili Skuli iweze kuchukua wanafunzi wengi kwa vile kwa sasa ni kinyanganyiro katika kisiwa hiki.
Pia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb) alitoa zawadi kwa walimu wa kidato cha 4, na walimu waliofaulisha zaidi katika masomo ya Hisabati, Kiengereza, Biology, Sayansi Jamii (Geography) na Chemistry Pamoja na kuwazawadia wasaidizi wa shule matron, patron na wapishi.