Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amepita baadhi ya maeno Jiji la Dar es Salaam kujionea namna Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vya Usalama wanavyotekeleza majukumu yao wakati Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati ukiendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere. Bashungwa wakati akipita katika maeneo ya Jiji hilo, leo tarehe 28 Januari 2025, amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP. Camillus Wambura kwa kuendelea kushirikiana na Vyombo vingine vya Serikali kuimarisha usalama katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, unaofanyika tarehe 27 na 28 Januari 2025. “Watanzania wameona nchini yetu ipo imara, tunamshukuru Rais na Amri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoendelea kuwezesha Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kuwa timamu muda wote kwa kukabiliana na jambo lolote na lenye ukubwa wowote” amesema Bashungwa. Bashungwa ameeleza kuwa Serikali inajivunia kazi nzuri inayoendel...
Marato tv - Sauti ya Jamii