Uwekezaji Ujenzi Ukumbi Wa Mikutano Ccm Mara Wafikia Asilimia 65

GEORGE MARATO TV
0


 

Na Shomari Binda-Musoma 

UWEKEZAJI wa ujenzi wa ukumbi mkubwa wa mikutano unaojengwa na Chama cha Mapinduzi ( CCM) mkoa wa Mara umefikia asilimia 65.

Hayo yamesemwa na Katibu wa chama hicho mkoa wa Mara Ibrahim Mjanakher alipokuwa akifanya mahojiano maalum na GMTV.

Amesema hadi ukumbi huo kufikia hapo ni juhudi za wanachama na wadau mbalimbali wa chama hicho mkoani Mara na nje ya mkoa wa Mara.

Mjanakher amesema hadi sasa zaidi ya milioni 700 zimetumika kwenye ujenzi huo unaotarajiwa kuchukua watu zaidi ya 2000 kwa wakati mmoja.

Amesema uwekezaji wa ukumbi huo ni maelekezo ya chama ngazi ya Taifa chini ya Mwenyekiti Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kutaka chama kuwa na miradi kila ngazi ili kiweze kujiendesha.

Katibu huyo amesema ujenzi wa ukumbi huo una simamiwa vixuri chini ya Mwenyekiti wa mkoa wa CCM Patrick Chandi chini ya kamati ya ujenzi inayoongozwa na Mwita Gachuma.

" Nashukuru ndugu Mwandishi kwa kutembelea hapa ofisini na kuona maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa mikutano unaoendelea.

" Ujenzi unaendelea vizuri kama ulivyoona na huu ni uwekezaji unaotokana na maelekezo ya chama taifa baada ya kupokea mara moja tukaanza ujenzi",amesema

Amesema katika hatua ya ujenzi uliofikia bado michango ya wanachama inajitajika ili kuweza kukamilisha hatua mbalimbali zilizobakia.

Ameongeza kuwa ukumbi huo unatarajiwa kukamilika mwezi wa 4 mwaka huu na kuanza kutoa huduma na michango ya vifaa inaendelea kupokelewa kwenye ofisi yake na fedha kuna namba maalum kwaajili ya mfuko wa uchangiaji wa miradi ya chama na kuwashukuru wale wote ambao wamechangia ujenzi huo hadi ulipofikia.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top