Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Bashungwa aingia Mtaani Kujionea Polisi Ilivyoimarisha Usalama Mkutano wa Nishati - Dar

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa   amepita baadhi ya maeno Jiji la Dar es Salaam kujionea namna Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vya Usalama wanavyotekeleza majukumu yao wakati Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati ukiendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere. Bashungwa wakati akipita katika maeneo ya Jiji hilo, leo tarehe 28 Januari 2025, amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP. Camillus Wambura kwa kuendelea kushirikiana na Vyombo vingine vya Serikali kuimarisha usalama katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, unaofanyika tarehe 27 na 28 Januari 2025.  “Watanzania wameona nchini yetu ipo imara, tunamshukuru Rais na Amri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoendelea kuwezesha Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kuwa timamu muda wote kwa kukabiliana na jambo lolote na lenye ukubwa wowote” amesema Bashungwa. Bashungwa ameeleza kuwa Serikali inajivunia kazi nzuri inayoendel...

Uwekezaji Ujenzi Ukumbi Wa Mikutano Ccm Mara Wafikia Asilimia 65

  Na Shomari Binda-Musoma  UWEKEZAJI wa ujenzi wa ukumbi mkubwa wa mikutano unaojengwa na Chama cha Mapinduzi ( CCM) mkoa wa Mara umefikia asilimia 65. Hayo yamesemwa na Katibu wa chama hicho mkoa wa Mara Ibrahim Mjanakher alipokuwa akifanya mahojiano maalum na GMTV. Amesema hadi ukumbi huo kufikia hapo ni juhudi za wanachama na wadau mbalimbali wa chama hicho mkoani Mara na nje ya mkoa wa Mara. Mjanakher amesema hadi sasa zaidi ya milioni 700 zimetumika kwenye ujenzi huo unaotarajiwa kuchukua watu zaidi ya 2000 kwa wakati mmoja. Amesema uwekezaji wa ukumbi huo ni maelekezo ya chama ngazi ya Taifa chini ya Mwenyekiti Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kutaka chama kuwa na miradi kila ngazi ili kiweze kujiendesha. Katibu huyo amesema ujenzi wa ukumbi huo una simamiwa vixuri chini ya Mwenyekiti wa mkoa wa CCM Patrick Chandi chini ya kamati ya ujenzi inayoongozwa na Mwita Gachuma. " Nashukuru ndugu Mwandishi kwa kutembelea hapa ofisini na kuona maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa mikutano u...

Waziri Mkuu ashiriki mkutano wa kumi na nane wa Bunge

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshiriki Mkutano wa kumi na nane wa bunge ulioanza leo Januari 28, 2025, bungeni jijini Dodoma. Mkutano huo ni mahsusi kwa ajili ya Kamati za Kudumu za Bunge kuwasilisha Taarifa za Mwaka za shughuli za kamati kwa kipindi cha Januari 2024 hadi Januari 2025.

Kazi Za Madiwani Viti Maalum Manispaa Ya Musoma Zapokelewa Na Waǰumbe Baraza Uwt

Na Shomari Binda-Musoma  KAZI zinazofanywa na madiwani wa viti maalum manispaa ya Musoma zimepokelewa na kupongezwa na wajumbe wa Baraza la UWT Wilaya ya Musoma mjini. Wakizungumza mara baada ya madiwani 5  kuwasilisha taarifa zao za kazi kuanzia januari 2023 hadi disemba 2024 wamesema wanaridhishwa na kazi zao.  Wajumbe hao ambao ni Mwenyekiti na Katibu kutoka Kata 16 za manispaa ya Musoma wamesema kilichowasilishwa na madiwani hao wameyakubali maana yalifanyika kwenye Kata zao Wamesema uhamasishaji wa vikundi waliufanya na vikundi kuanzishwa na vingine tayari vimeshapata mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri ya manispaa ya Musoma.  Kwa kauli moja wajumbe hao wamesema wanapokea kazi walizofanya kwa mikono miwili na wametekeleza majukumu yao. " Mwenyekiti tumepokea taarifa za madiwani wetu na tunazipokea kwa mikono miwili maana kazi walizozifanya tumeziona na tumewaona kwenye Kata zetu",wamesema. Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Musoma Stera Mtani amewapongeza ...

Watanzania Wanaotafuta Kazi Nje ya Nchi Zingatieni Sheria-Kikwete

Na. Mwandishi wetu - Saudi Arabia.  Serikali imekemea watanzania wanao kwenda kufanya kazi nje ya nchi bila kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria kwa kuwa inasababisha kutojulikana walipo na shughuli wanazozifanya. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi  ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wa uzinduzi wa utekelezaji wa makubaliano ya kuwezesha na kuratibu Ajira za Watanzania nchini Saudi Arabia leo Januari 27. 2024. (Tuseme ni wapi ameyasema hayo) Aidha, amesema uhusiano mazuri uliopo baina ya Tanzania na nchi ya Saudi Arabia hawataruhusu wafanyakazi kufanya kazi au kusafiri bila kufuata utaratibu, hivyo kila mtanzania anayehitaji kufanya kazi nje ya nchi apitie kwa mawakala wanatambulika baina ya nchi hizo mbili. Mhe. Ridhiwani amesema miongoni mwa makubaliano yaliyofikiwa ni pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa watanzania kusafiri kwenda nchini Saudi Arabia, upimaji wa Afya zao, kupata kazi zenye staha na mshahar...

Dkt.Biteko awapa pole Bukombe kufuatia ajali ya radi.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa pole kwa wananchi wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita kufuatia ajali ya radi iliyotokea leo Januari 27, 2025 katika Kata ya Ushirombo. Sehemu ya taarifa hiyo salamu za pole ya Dkt. Biteko iliyotolewa leo Januari 27, 2025 inaeleza kuwa ajali hiyo ya radi imesababisha vifo vya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Businda. “ Nimepokea taarifa ya vifo vya watoto wetu wa Businda Sekondari kwa masikitiko makubwa. Naomba kuwapa pole sana wazazi, walezi, walimu, wanafunzi wa shule hii na ndugu wote waliguswa na msiba huu mkubwa,” amesema Dkt. Biteko. Ameendelea “Vifo vya vijana wetu vimetushtua sana wana Bukombe wote. Tunawaombea faraja familia zote zilizofikwa na msiba huu aidha, tunawaombea uponyaji wa haraka majeruhi wote kwenye kadhia hii.” Aidha, Dkt. Biteko ameelekeza Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na Ofisi ya Mbunge kufuatilia kwa karibu matibabu ya majer...