Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Serikali yaipa kongole kampuni ya CRJE ikiahidi kuendelea kudumisha mahusiano mema na China

  Na Mwandishi Wetu SERIKALI imeipongeza Kampuni ya ukandarasi kutoka nchini China ya CRJE (East Africa) Ltd kwa ufanyaji kazi uliotukuka huku ikiahidi kuendelea kukuza mahusiano yaliyodumu kwa muda mrefu kati ya Tanzania na China Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Katiba na Sheria Dk Damas Ndumbaro wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Uwajibikaji kwa Jamii ya CRJE kwa ushirikiano na Hoteli ya Johari Rotana. Hafla hiyo ilihudhuliwa na wageni mbalimbali akiwemo, John Mnali, Mkurugenzi wa Ukuzaji Uwekezaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mwenyekiti wa Mwalimu Nyerere Foundation Joseph Butiku na balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian Akizungumza kwa niaba ya Waziri Ndumbaro, ofisa mwandamizi katika wizara hiyo Shoma Philip Ndono, alisema Kampuni ya CRJE imeongeza kwa kiasi kikubwa uhusiano mwema wa urafiki kati ya China na Tanzania. "Tunashukuru na tunatamani urafiki wetu uendelee kudumu kwa muda mrefu ujao.”Alisema kampuni hiyo ya ukandarasi kutoka China ...

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali John Mkunda apokea Tuzo

   Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda akipokea Tuzo iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Iringa kutambua mchango wake katika mafanikio na ukuaji wa Chuo hicho  kutoka kwa Mkuu wa Utumishi Jeshini Meja Jenerali Marco Elisha Gaguti aliyeipokea kwa niaba yake.

Wataalam wa Ununuzi na Ugavi Chukieni Rushwa, Fanyeni Kazi Kwa Uwazi-Dkt. Biteko

 *📌 Atahadharisha vitendo vya rushwa kwenye Manunuzi* *📌 Dkt. Biteko afungua Kongamano la 15 la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi* *📌 Ataka wasikilize sauti za watu, kutathimini utendaji kitaaluma* *Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati* Naibu Waziri Mkuu na  Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka wataalam wa ununuzi na ugavi nchini kizingatia misingi ya maadili ya taaluma yao ili kuiwezesha Serikali kuleta maendeleo kwa wananchi wake. Dkt. Biteko amesema hayo leo Desemba 17, 2024 wakati akifungua Kongamano la 15 la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi linaloendelea Jijini Arusha. Amesema wataalam wa ununuzi na ugavi ni muhimu katika kuchagiza maendeleo na Serikali inawategemea ili kufanikisha mipango yake. “ Wataalam wa manunuzi na ugavi mna mchango mkubwa, zaidi ya asilimia 70 ya bajeti nzima ni kwa ajili ya manunuzi, hivyo kuweni waadilifu, Chukieni Rushwa na kushauri namna bora ya kufanikisha mipango ya Maendeleo” amesema Dkt. Biteko. Amesema kutokana na uku...

Benki ya Dunia yaipongeza Tanzania Mradi wa sgr

Benki ya Dunia imeshangazwa na hatua kubwa iliyofikiwa na Serikali katika kutekeleza Mradi wa Kimkakati wa Reli ya Kisasa wa SGR, na kuahidi kuwa itaweka mkono wake kusaidia ujenzi wa Reli hiyo muhimu kwa kukuza biashara na ukuaji wa uchumi wa nchi. Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam, na Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Benki ya Dunia anayesimamia Ujenzi wa Miundombinu, Bi. Wendy Hughes, aliyepo nchini kwa ziara ya kikazi, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mawaziri watatu wa Kisekta, wakiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. Abdallah Ulega. Bi. Hughes aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Bw. Nathan Belete na Viongozi wengine waandamizi wa Benki hiyo, alisema kuwa amesafiri kwa kutumia reli hiyo kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma na kushangazwa na kiwango cha ubora wake wa viwango vya kimataifa. Alisema kuwa Benki ya Dunia inaendelea kuchakata maombi yaliyowasilishwa na...

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali John Mkunda apokea Tuzo

 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda akipokea Tuzo iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Iringa kutambua mchango wake katika mafanikio na ukuaji wa Chuo hicho  kutoka kwa Mkuu wa Utumishi Jeshini Meja Jenerali Marco Elisha Gaguti aliyeipokea kwa niaba yake.

Tcra yaanza kuwanoa waandishi wa habari maandalizi ya uchaguzi mkuu 2025

  Na Angela Sebastian Bukoba  Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka waandishi na vyombo vya habari kuandika habari kwa kufuata sheria,kanuni na taratibu za uchaguzi tunapoelekea uchaguzi mkuu kwa ajili ya usalama wa Taifa letu na wananchi wake. Mhandisi Kadaya Baluhye meneja wa kitengo cha watumiaji huduma masuala ya mawasiliano kutoka TCRA makao makuu ametoa ushauri huo wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Kagera, kutoka vyombo mbalimbali vya habari ambayo yamefanyika mjini Bukoba. Mhandisi Baluhye amesema kuwa kufuata kanununi na sheria za uchaguzi zinampa mwandishi mwongozo wa namna ya kuandika au kuendesha vipindi kwa usahii na usalama. "Mwaka kesho ni uchaguzi mkuu ambao unagusa uchaguzi wadiwani,wabunge na Rais kwa kushirikisha vyama mbalimbali hivyo tuwe makini kwa kufuata kanununi,sheria na taratibu za uchaguzi na kutopendelea na kuweka ushabiki wa vyama mbele ili kulinda usalama wetu na nchi yetu maana wapo baadhi yetu wanatum...