Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Majaliwa ahitimisha Jimbo Cup Ruangwa

*_Kiwengwa FC yaibuka bingwa wa michuano hiyo._* Waziri Mkuu na Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Kassim Majaliwa ameshuhudia mchezo wa fainali ya kombe la jimbo maarufu Jimbo cup kati ya Stand fc na Kiwengwa FC uliofanyika katika uwanja wa mpira wa miguu wa Majaliwa, Ruangwa Mkoani Lindi. Katika mchezo huo uliopigwa Novemba 25, 2024, timu ya kiwengwa Fc iliibuka bingwa baada ya kuwatandika Stand Fc kwa mikwaju ya Penati 4-1. Akizungumza baada ya mchezo huo Mheshimiwa Majaliwa amesema michezo hiyo inatumika kuboresha maendeleo ya mpira wa miguu katika wilaya hiyo. “Nitazungumza na chama cha makocha Taifa ili watupatie wakufunzi ambao watakuja kuwapa mafunzo makocha wa wilaya ya Ruangwa ya namna bora ya kusimamia timu zetu” Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amesema kwa kuwa Wilaya ya Ruangwa imeamua kujidhatiti kwenye mpira wa miguu ni muhimu kuwa na waamuzi wenye uwezo mkubwa wa kusimamia michezo “Chama cha Mpira cha Wilaya orodhesheni marefa waliopo katika wilaya hii, nitaomba uongozi wa marefa tup...

Shemsa asisitiza Umuhimu wa Uchaguzi Katika Maendeleo

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu Ndg.Shemsa Mohamed ameendelea na ziara yake yenye jina la *Siku Saba za Moto* ambapo tarehe 25 Novemba, 2024 aliweka kambi katika Jimbo la Kisesa akitembelea Kata ya Bomani ,Kata ya Isengwa na Mwasengela . Ndg.Shemsa amekutana na kuzungumza na  makundi mbalimbali ya Wananchi katika  Jimbo la Kisesa huku akisisitiza Wananchi kukichagua Chama Cha Mapinduzi kwani ndicho Chama kilichojitanabaisha katika uongozi na utumishi kwa Umma . Katika Ziara hiyo Ndg.Shemsa Mohamed amesisitiza umuhimu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mustakabali wa Maendeleo ya Vijiji na Taifa kwa ujumla na kuwataka Wananchi kutumia vyema haki yao ya kuchagua viongozi bora walioandaliwa na Chama Cha Mapinduzi . Mwisho Ndg.Shemsa Mohamed ,Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu amewataka wanachama wa CCM na Wananchi kwa ujumla kuendelea na kampeni kwa ustaarabu na amani na kujitokeza tarehe 27 kutumia haki yao ya kupiga kura katika hali ya amani na ...

Taifa Stars Yapigwa Faini ya Shilingi Millioni 132

CAF imethibitisha kuwa Tanzania itashiriki michuano ijayo ya AFCON  2025 lakini Tanzania imepigwa faini ya USD 50000 (Tshs 132m) kwa kosa la Mchezaji wao kutumia namba mbili tofauti Pia CAF imetupilia mbali malalamiko ya Shirikisho la Soka la Guinea kuhusu ombi lao la kuhitaji Tanzania iondolewe katika michuano ya AFCON 2025 kutokana na Mchezaji wao kutumia namba mbili tofauti.

Mbunge Mathayo akabidhi Gari la Wagonjwa Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere

Na Shomari Binda-Musoma MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amekabidhi gari ya kubebea wagonjwa kwenye hospital ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliuopo Musoma Akizungumza hospitalini hapo na madaktari,wauguzi na watumishi amesema gari hiyo ni sehemu ya mgao wa serikali katika kutoa vitendea kazi na vifaa tiba. Amesema serikali imekuwa ikitoa vifaa mbalimbali na safari hii wameongeza gari kwaajili ya kubeba wagonjwa. Mathayo amesema serikali pia imekuwa ikiendelea kutoa fedha nyingi kwaajili ya kuendeleza ujenzi wa hospital ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ili kutoa tiba za kibingwa. " Tunaishukuru sana serikali yetu chini ya Dkt.Samia Suluhu Hasani kwa kutuongezea gari hili kwaajili ya kutoa huduma kwa wananchi wetu. " Lakini pia serikali imekuwa ikitoa na kutuletea vifaa tiba na kutoa fedha nyingi kwaajili ya muendelezo wa ujenzi,tunamshukuru sana mheshimiwa Rais",amesema. Mathayo amesema wataendelea kuiomba serikali vifaa katika huduma ya afya ikiwa ni ku...

Tunataka Maendeleo Kwa ajili ya Watu Wetu-Dkt. Biteko

*📌 Ahimiza Watanzania Kujitokeza  Kupiga Kura Novemba 27* *📌 Awaomba Wananchi wa Namonge Kuchagua Wagombea wa CCM* Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024, CCM imedhamiria kuendelea kutekeleza miradi  ya maendeleo ili kubadilisha hali za maisha ya wananchi. Amesema Kata ya Namonge ni kati ya kata  17 za Wilaya ya Bukombe yenye vijiji vinane na vitongoji 36 ambayo imeendelea kupiga hatua ya maendeleo kwa kuwa na mtandao mrefu zaidi wa barabara kuliko kata zingine. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 25, 2024 wakati akihutubia katika Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wilayani Bukombe zilizofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Namonge mkoani Geita. “ Tunataka maendeleo kwa ajili ya watu wetu na kata hii imeandikisha idadi kubwa ya wananchi leo nimekuja kuwaomba mchague viongozi wa CCM ili tuend...

Mbunge Mathayo"Apoi"Aendelea Kuwatafutia Kura Wenyeviti wa Mitaa Ccm

Na Shomari Binda-Musoma MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini,Vedastus Mathayo " apoi" akiendelea kulizunguka jimbo la Musoma mjini kuwatafutia kura Wenyeviti na wajumbe kutoka Chama cha Mapinduzi. Tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa novemba 20 mbunge huyo kwa kushirikiana na viongozi wa CCM wamekuwa wakipita kwenye mitaa kuwatafutia kura wagombea hao. Leo novemba 25 mbunge huyo atanzuguka kwenye mitaa ya Makoko,Mwisenge na Nyasho katika muendelezo wa kutafuta kura za wagombea hao.  Akizungumza na GMTV mwenendo wa kampeni hizo mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amesema anauona ushindi wa wagombea wa CCM kwa kuwa wamesimamisha wagombea safi na wanao kubalika. Amesema kila alupipita kuomba kura kwenye mitaa mbalimbali wananchi wamemuakikishia kuwachagua wagombea hao. " Kwa muda mfupi wa kampeni nimepita mitaa mbalimbali kuwaombea kura wagombea wa CCM na wananchi wameahidi kutuchagua. " Niwahakikishie wananchi mitaa yote 73 ya jimbo la Mus...