Na Shomari Binda-Musoma
MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amekabidhi gari ya kubebea wagonjwa kwenye hospital ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliuopo Musoma
Akizungumza hospitalini hapo na madaktari,wauguzi na watumishi amesema gari hiyo ni sehemu ya mgao wa serikali katika kutoa vitendea kazi na vifaa tiba.
Amesema serikali imekuwa ikitoa vifaa mbalimbali na safari hii wameongeza gari kwaajili ya kubeba wagonjwa.
Mathayo amesema serikali pia imekuwa ikiendelea kutoa fedha nyingi kwaajili ya kuendeleza ujenzi wa hospital ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ili kutoa tiba za kibingwa.
" Tunaishukuru sana serikali yetu chini ya Dkt.Samia Suluhu Hasani kwa kutuongezea gari hili kwaajili ya kutoa huduma kwa wananchi wetu.
" Lakini pia serikali imekuwa ikitoa na kutuletea vifaa tiba na kutoa fedha nyingi kwaajili ya muendelezo wa ujenzi,tunamshukuru sana mheshimiwa Rais",amesema.
Mathayo amesema wataendelea kuiomba serikali vifaa katika huduma ya afya ikiwa ni kuiombea na hospital ya mznispaa ya Musoma.
Akitoa shukrani baada ya kupokea gari hilo mganga mfawidhi wa hospital hiyo Dk.Osmund Dyagura amemshukuru mbunge huyo kwa kuwa mfatiliajj wa vifaa vya huduma ya afya na kuwafikia.
Amesema serikali inatoa vifaa nchi nzima na mbunge anapokuwa karibu wizarani ni rahisi vifaa kufika kwa wakati na kuwahudumia wananchi.




Comments
Post a Comment