Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Balozi Nchimbi ateta na ujumbe kutoka nchini comoro

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi amekutana na Mheshimiwa Youssoufa Mohamed Ali,Waziri wa Ulinzi ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama Tawala Comoro cha CRC ambaye pia ni Katibu wa Rais wa Umoja wa Visiwa vya Comoro. Katika mazungumzo ya viongozi hao yamelenga kuimarisha uhusiano baina ya vyama hivyo ikiwa ni pamoja na kutoa fursa za mafunzo kwa watendaji wa Chama cha CRC nchini Tanzania. Aidha viongozi hao wamepongeza juhudi za ushirikiano wa nchi hizo mbili unaofanywa na Marais wake Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan na Mheshimiwa Azali Assoumani. Ziara hiyo imeratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro,Mheshimiwa Youssoufa anatarajiwa pia kutembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete,Shirika la Uzalishaji Mali SUMA JKT na pia Taasisi binafsi kadhaa zenye dhamira ya kuwekeza nchini Comoro.

Mwigobero na Mukendo kufungua mathayo cup 2024 jumapili uwanja wa posta musoma

Na Shomari Binda-Musoma MASHINDANO ya kombe la Mathayo Cup 2024 yanaanza kutimua vumbi kesho novemba 3 kwenye ueanja wa Posta manispaa ya Musoma. Mathayo Cup yamekuwa yakiandaliwa kila mwaka na mbunge wa jimbo LA Musoma mjini Vedastus Mathayo na yamekuwa na hamasa kubwa. Kesho kwenye ufunguzi mashindano hayo yatafunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Issa Chikoka akiwa na Meya wa manispaa ya Musoma Patrick Gumbo. Michezo 2 ya ufunguzi itachezwa ambapo mapema saa 8 utachezwa mchezo kati ya Mwigobero na Mukendo na baadae saa 10 itakuwa zamu ya Iringo ns Kitaji. Katibu wa mbunge Mathayo Seti Maendaenda amesema maandalizi yote yamekamilika ikiweo timu kupewa vifaa ikiwemo seti ya jezi. Seti amesema mashindano ya mwaka huu yameonekana yatakuwa na ushindani kutokana na kila timu kujiandaa vizuri. " Kila kitu kimekamilika kwaajili ya mashindano ya Mathayo Cup 2024 na yanakwenda kuanza kesho novemba 3. " Tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanja wa Posta kwenye ufunguzi wa...

Kumalizika kwa mkataba wa ununuzi wa umeme kati ya Tanesco na kampuni ya songas

 Mkataba wa ununuzi wa umeme kati ya shirika la ugavi wa umeme nchini (TANESCO) na Kampuni ya uzalishaji umeme kwa  njia ya gesi asilia ya Songas umefikia tamati. Kumalizika kwa mkataba huo kumetokana na maendeleo mazuri ya mradi wa bwawa la kufua umeme la Julius nyerere  ambalo mpaka sasa Jumla ya megawatimegawati 940 zimeungwa kwenye Grid ya taifa Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano na uhusiano Tanesco Makao makuu imewahakikishia wateja kuwa hali ya upatikanaji wa nishati ya umeme itaendelea kuimarika kwa kuzingatia vyanzo mbalimbali vya uzalishaji umeme.  Taarifa hiyo imeeleza kuwa kwa sasa uwezo wa uzalishaji umeme kwa kutumia mitambo ya gesi asilia na mitambo inayotumia maji ni mkubwa kuliko mahitaji ya umeme hapa nchini Serikali kupitia wizara ya nishati na Tanesco imeahidi kuendelea kusimamia kikamilifu sekta ndogo ya umeme ili kuhakikisha kunakuwa na huduma bora,endelevu na ya uhakika.

Wasifu wa Jenerali mstaafu David Musuguri

  Jenerali mstaafu David Bugozi Waryoba Musuguri alizaliwa Januari 4, ‌1920 katika Kijiji cha Kumuruti,Masabha.Sasa sehemu hiyo inajulikana kama Nyasirori, akiwa mtoto wa tatu katika familia ya mzee Musuguri wa Nzangho. Alipozaliwa aliitwa jina la Waryoba,ikiwa ni ishara kwamba alizaliwa asubuhi wakati jua linachomoza. Baba yake mkubwa, Mgendi wa Nzangho alimwita jina la Bugingo. Akiwa na umri wa miaka mitano, mzee Musuguri Nzangho alihamia Kijiji cha Butiama‌, ‌wakati huo paliitwa ‌Mu-kyaro. Jenerali mstaafu David Bugozi Waryoba Musuguri alikuwa mtoto wa tatu kuzaliwa katika tumbo la mama yake, Wakuru wa Kibumbiko.Bibi mzaa mama yake pia alikuwa anaitwa Wakuru wa Kigeso. Jina la Wakuru ni jina kubwa sana katika ukoo huu wa Jenerali Musuguri. Mzee Musuguri wa Nzangho alioa wanawake ‌sita. Alikuwa mfugaji wa ng’ombe na mbuzi na alikuwa stadi kulinda mifugo yake, kwani yeye na wachungaji wenziwe waliwahi kwenda kuwinda simba na waliua simba 18‌. Enzi hizo wanyamapori walikuwa wapo ma...

Makamu wa Rais amewataka makamanda na wapiganaji wa Jwtz kuiga mfano wa Jenerali Musuguri

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema katika kumuenzi Jenerali Mstaafu David Musuguri inapaswa Watanzania wote yaani askari na raia kujitoa, hata ikibidi kufa kwa ajili ya kulinda na kutetea uhuru, heshima na maslahi ya Taifa. Makamu wa Rais amesema hayo leo Novemba 01-2024 wakati wa kuaga mwili wa Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali David Bugozi Musuguri katika viwanja vya Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo Jijini Dar es salaam.  Ametoa rai hasa kwa vijana wa Tanzania kuipenda nchi na jeshi la Tanzania kwa moyo wote na kuwa tayari kuilinda Tanzania kwa gharama yoyote kama alivyofanya Jenerali (Mstaafu) Musuguri. Makamu wa Rais amesema Makamanda na Wapiganaji waliopewa dhamana ya uongozi katika Jeshi hawana budi kuendelea kufuata mfano bora uliyoachwa na Jenerali Mstaafu David Musuguri. Amesema Hayati Jenerali (Mstaafu) Musuguri alilipenda sana Jeshi maisha yake yote ambapo alitamani vijana wengi wajiunge na Jeshi na alifanikiwa sana kuwaandikis...

Wazazi wamshukuru mbunge Mavunde kwa ujenzi wa uzio shule ya msingi uhuru-dodoma

▪️Shule ina umri wa miaka 96 tangu kuanzishwa kwake ▪️Muingiliano wa masomo na biashara kuzunguka Shule ilikuwa kikwazo ▪️Wanafunzi washukuru kuhakikishiwa Usalama wao ▪️Mbunge Mavunde amshukuru Rais Samia kwa madarasa 📍Dodoma Wananchi na wazazi wa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru Jijini Dodoma, wamempongeza na kumshukuru Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini *Mh. Anthony Mavunde* kwa ufadhili wa ujenzi wa uzio wa shule hiyo ili kuboresha mazingira rafiki ya wanafunzi kusomea tofauti na awali ambapo muingiliano ulikuwa mkubwa kati ya wafanyabiashara wanaozunguka eneo la shule na shughuli za masomo za wanafunzi. Wakitoa shukrani zake leo wakati wa hafla ya kukabidhi uzio huo,Mwenyekiti wa Kamati ya wazazi wa Shule ya Uhuru *Ndg. Aman Sadick* na Mwenyekiti wa CCM kata  *Ndg. Rashid Said Gwazae* wamesema moja ya changamoto kubwa iliyokuwa inawakabili wanafunzi katika eneo hilo ni juu ya usalama wao na kukosa utulivu wakati wa masomo na hivyo kumshukuru Mbunge Mavunde kutatua kero hii ili...