Kumalizika kwa mkataba wa ununuzi wa umeme kati ya Tanesco na kampuni ya songas

GEORGE MARATO TV
0



 Mkataba wa ununuzi wa umeme kati ya shirika la ugavi wa umeme nchini (TANESCO) na Kampuni ya uzalishaji umeme kwa  njia ya gesi asilia ya Songas umefikia tamati.

Kumalizika kwa mkataba huo kumetokana na maendeleo mazuri ya mradi wa bwawa la kufua umeme la Julius nyerere  ambalo mpaka sasa Jumla ya megawatimegawati 940 zimeungwa kwenye Grid ya taifa

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya mawasiliano na uhusiano Tanesco Makao makuu imewahakikishia wateja kuwa hali ya upatikanaji wa nishati ya umeme itaendelea kuimarika kwa kuzingatia vyanzo mbalimbali vya uzalishaji umeme. 

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kwa sasa uwezo wa uzalishaji umeme kwa kutumia mitambo ya gesi asilia na mitambo inayotumia maji ni mkubwa kuliko mahitaji ya umeme hapa nchini

Serikali kupitia wizara ya nishati na Tanesco imeahidi kuendelea kusimamia kikamilifu sekta ndogo ya umeme ili kuhakikisha kunakuwa na huduma bora,endelevu na ya uhakika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top