Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wafanyabiashara dodoma wamshukuru Rais Samia kwa ujenzi wa machinga complex

▪️Jiji kujenga sakafu kupunguza nguvu ▪️Mbunge Mavunde awachangia 10m kutunisha mfuko wa Soko ▪️Awataka Mgambo wa Jiji kuacha kutumia mabavu ▪️Aahidi kuwaunganisha na Taasisi za fedha kwa ajili ya mitaji ▪️DC Shekimweri aahidi kusimamia utatuzi wa kero sokoni 𝐃𝐨𝐝𝐨𝐦𝐚 Wafanyabiashara wadogo wa Soko la Machinga Complex Jijini Dodoma wameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ilivyowahamisha kutoka barabarani na kuwajengea soko maalum maarufu kama Machinga Complex. Akizungumza katika mkutano mkuu wa soko Kaimu Mwenyekiti wa Machinga Complex Ndg. Lucas Kingamkono ameishukuru serikali kwa uwepo wa soko la Machinga ambalo limerahisisha ufanyaji wa biashara kwa wafanyabiashara hao wadogo ambao awali walikuwa maeneo ambayo hayakuwa rasmi na hivyo kufanya biashara kwa mashaka. Akizungumza katika mkutano huo,Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini *lMh. Anthony Mavunde ameupongeza uongozi wa soko Kwa kuandaa mkutano wa kusikiliza kero za wafanyabiash...

Mariam mwinyi apongeza jitihada za wake wa marais afrika

 Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mhe. Mama Mariam Mwinyi ameeleza kufurahishwa na mchango mkubwa wa wake wa Marais wa Afrika, hasa katika kutoa ufadhili wa masomo kwa fursa 2,080 kwa madaktari chipukizi kutoka nchi 52 za Afrika kwenye taaluma 44 muhimu zinazohitajika, kama vile “oncology,” utaalamu wa afya ya uzazi kwa kina mama, tiba ya kisukari, na magonjwa mengine. Mama Mariam Mwinyi, ameyasema hayo leo tarehe 29 Oktoba 2024 alipozungumza katika Mkutano wa 11 wa “Merck Foundation Africa Asia Luminary” uliofanyika katika hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam, uliowakutanisha wake wa Marais wa Afrika kutoka nchi 15. Aidha Mama Mariam Mwinyi ametumia fursa hiyo kuipongeza “Merck Foundation” kwa kutimiza miaka 12 ya utekelezaji wa miradi yake ya maendeleo kwa nchi za Afrika na Asia, pamoja na miaka saba tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo. Halikadhalika, Mama Mariam Mwinyi amepongeza jitihada za ...

Biteko kuongoza maafisa wa ngazi ya juu Jwtz,Maafisa wa kati, askari na watanzania kuaga mwili wa Jenerali mstaafu Musuguri lugalo 01.11.2024

 

Shule ya msingi twibhoki bagamoyo yang'ara matokeo ya darasa la saba 2024

 

Mkuu wa jeshi la kujenga taifa awapa pole viongozi na wachezaji wa Jkt tanzania fc

 Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Generali Rajabu Mabele amekutana ns kusalimiana na baadhi ya viongozi wa JKT Tanzania FC na wachezaji alipowatembelea kwa ajili ya kuwapa Pole. Meja Jenerali Mabele ambae amepokelewa na viongozi wa JKT Tanzania FC baada kuwasili katika kambi ya wachezaji, Mbweni, Dar Es salaam kuwajulia hali kutokana na ajali waliyoipata 27 October 2024 baada ya basi lao walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kuanguka eneo la Mbweni, wakitokea Dodoma kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji. Mkuu huyo wa JKT amepata nafasi ya kuzungumza na kuwapa Pole viongozi navwachezaji hao wa JKT Tanzania FC.

Mkuu wa majeshi nchini atangaza rasmi kifo cha Jenerali mstaafu David Musuguri