Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

AWESO ATEKELEZA MAAGIZO YA DKT NCHIMBI MISUNGWI AMUONDOA MENEJA WA RUWASA

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amemuondoa katika nafasi yake Meneja wa RUWASA wilayani Misungwi Mhandisi Marwa Kisibo kutokana na kutosimamia utekelezaji wa miradi ipasavyo katika wilaya yake. Waziri Aweso amefanya maamuzi hayo alipotembelea Mradi wa Maji wa Ukiliguru - Usagara - Kolomije - Sumve wa Chanzo cha Ziwa Victoria unaogharimu kiasi cha zaidi ya Bilioni 32 wilayani Misungwi na Kwimba Mkoa wa Mwanza. Ziara hii ni Maelekezo ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Dkt Emmanuel Nchimbi alipofanya ziara yake mkoani Mwanza wilaya ya Simiyu na kupata malalamiko ya hali ya upatikanaji Maji na kusuasua kwa Miradi. Dkt Nchimbi alimuelekeza Aweso kufika Misungwi na kufanyia kazi changamoto zote Katika ziara hiyo, Mhe Aweso ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri. Mradi huu utanufaisha vijiji 19 wilaya ya Misungwi na vijiji 5 vya wilaya ya Kwimba vyenye jumla ya watu 85,400 na kuondoa kero ya maji katika maeneo makubwa ya Usagara na Nyashishi. Aidha Aweso ...

DC Chikoka Aanza Mkakati wa Kuipandisha Timu ya Biashara United Ligi Kuu Msimu Ujao

Na Shomari Binda-Musoma MKUU wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amesema msimu huu mkoa wa Mara una jambo lake moja la kuhakikisha timu ya Biashara United inapanda ligi kuu msimu ujao. Kauli hiyo ameitoa septemba 8 kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma kwenye tamasha la kuwatambulisha wachezaji na benchi la ufundi la timu hiyo maarufu kama " Kichuri Day". Amesema baada ya kushindwa kupanda ligi kuu msimu uliopita sasa msimu huu jambo ni moja kuhakikisha lengo linatimia Chikoka amesema kupanda kwa timu hiyo kutatokana na ushirikiano wa pamoja baina ya timu na wadau wote wa mkoa wa Mara. Amesema imempendeza Rais Dkt.Samia kumleta Musoma na kuomba ushirikiano kwa wana Musoma na mkoa wa Mara kiujumla kuhakikisha Biashara United inapanda ligi kuu msimu ujao. " Msimu huu jambo ni moja tu kuhakikisha Biashara United inapanda ligi kuu msimu ujao na hili litafanikiwa iwapo tutashirikiana kwa pamoja. Tukishirikiana kwa pamoja kuanzia mwanzo wa msimu hakuna jambo litakaloshindikana tut...

Mhe. Kikwete Ashiriki Mapokezi ya Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi Taifa

Mbunge wa jimbo la Chalinze  ambaye pia ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi,vijana,Ajira na wenye Ulemavu Mh Ridhwani Jakaya Mrisho Kikwete Septemba 8 ameshiriki kumpokea  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Cde Ally Salum Hapi wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. Mh Kikwete ameitumia ziaza hiyo kueleza mafanikio ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi 2020-2025 huju aki kuwakumbusha wananchi kujiandikisha katika daftari la ukaazi na kupiga kura. Aidha mbunge huyo wa Chalinze pia  amewahimiza wananchi kuendelea kuamini kuwa serikali ya CCM chini ya Uongozi wa Rais  Dr Samia Suluhu Hassan na kwamba Serikali bado inaendelea kutekeleza majukumu yake na yanakwenda vizuri hivyo wana kila sababu ya kuendelea kumuunga mkono Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MFANYAKAZI WA PREMER CASINO MWANZA AILILIA SERIKALI

  MFANYAKAZI WA PREMER CASKNO MWANZA AILILIA SERIKALI. Na Mwandishi Wetu, Mwanza MFANYAKAZI wa Premer Casino ya Mwanza katika Idara ya Ulinzi Bw Nassor Butondo amelalamikia kitendo cha kushambuliwa na wachina Agosti ak 30, mwaka huu, majira ya usiku wakati anatekeleza majukumu yake ya ulinzi, Jambo Digital imeelezwa. Aidha Butondo ameulalamikia uongozi wa Casino hiyo iliyoko katika Jengo la Rock City Mall Wilayani Ilemela kwa kushindwa kumhudumia kimatibabu mlinzi wao huku wakitumia fedha nyingi kuwatibisha wachina walioanzisha fujo ndani ya Casino. "Mwajili wangu anawathamini zaidi wachina kuliko mimi, ndio maana pengine ni kwasababu ndio wateja wa kamali, hivyo matusi yao ya nguoni inabidi wafanyakazi wayavumilie tu, wakati mwingine huwadhalilisha wafanyakazi wa kike kwa kuwaingizia vidole sehemu ambazo sio rasmi, Serikali itusaidie" alifafanua Butondo. Imedaiwa kuwa siku hiyo kulitokea kutoelewana kati ya mchina na mzungu baada ya mchina (jina tunalo) kuliwa kwenye ...

Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato Dodoma Wafikia Asilimia 72

Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato uliopo jijini Dodoma umefikia hatua ya asilimia 72 katika ujenzi wa barabara ya kuruka na kutua ndege, wakati jengo la abiria likiwa limekamilika kwa asilimia 39.

SERIKALI KUJENGA SKIMU YA UMWAGILIAJI WILAYANI IRAMBA

  Tume ya Taifa ya Umwagiliaji(NIRC) imewaelekeza wataalam wake kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya kupata mahali pa kujenga skimu ya Umwagiliaji katika bonde la Ulemo-Nzinziligi-Mbelekese lililopo wilayani Iramba Mkoani Singida. Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Raymond Mndolwa ametoa maelekezo hayo wilayani Iramba wakati akimuonesha Waziri wa Fedha Dokta.Mwigulu Nchemba ramani ya Jiografia ya Bonde hilo. Kwa mujibu wa Mndolwa,Baada ya kukamilika kwa upembuzi yakinifu,Serikali itajenga Skimu ya Umwagiliaji katika bonde hilo utakaohusisha Bwawa,uchimbaji wa visima pamoja na Miundombinu ya umwagiliaji. Bonde la Ulemo-Nzinziligi-Mbelekese lina ukubwa wa hekta 43,000 ambapo Ujenzi wa skimu ya Umwagiliaji unatarajia kunufaisha wakulima katika kata sita za Ulemo,Ndago,Mbelekese,Mukulu, Kaselya pamoja na Kiengege.