Mbunge wa jimbo la Chalinze ambaye pia ni waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi,vijana,Ajira na wenye Ulemavu Mh Ridhwani Jakaya Mrisho Kikwete Septemba 8 ameshiriki kumpokea Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Cde Ally Salum Hapi wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
![]() |
Mh Kikwete ameitumia ziaza hiyo kueleza mafanikio ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi 2020-2025 huju aki kuwakumbusha wananchi kujiandikisha katika daftari la ukaazi na kupiga kura.
Aidha mbunge huyo wa Chalinze pia amewahimiza wananchi kuendelea kuamini kuwa serikali ya CCM chini ya Uongozi wa Rais Dr Samia Suluhu Hassan na kwamba Serikali bado inaendelea kutekeleza majukumu yake na yanakwenda vizuri hivyo wana kila sababu ya kuendelea kumuunga mkono Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.