Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt Mwinyi: Zanzibar Kushirikiana na Wasanii Kutangaza Vivutio

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Wasanii kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii. Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na Mwanamuziki kizazi kipya Omary Ally Mwanga maarufu Marioo , Ikulu Zanzibar tarehe 22 Julai 2024. Aidha Rais Dkt.Mwinyi amempongeza Marioo kwa kazi nzuri ya kuitangaza Tanzania kupitia kazi yake ya muziki. Naye Marioo ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa fursa aliyoipata ya kurekodi wimbo wake mpya wa Hakuna Matata katika mazingira ya vivutio vya Zanzibar . Pia amempongeza Rais Dkt.Mwinyi kwa jitihada zake kubwa za kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.

Biden Ajitoa Kwenye Kinyang'anyiro Cha Urais Marekani

BBC News,  Swah Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza kusitisha kampeni za kuwania muhula wa pili wa na kusema kusema amechukua uamuzi huo ''kwa maslahi ya chama chake na nchi.'' Uamuzi wa Biden kujitoa kwenye mbio za urais huku ikiwa imesalia miezi minne pekee kabla ya Wamarekani kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu. Kwa wiki kadhaa sasa Biden amekuwa akishinikizwa ajitoe kwenye kinyang’anyiro hicho na wanachama wenzake wa chama cha Democrats baada ya kufanya vibaya kwenye mjadala na mgombea wa chama cha Republican Donald Trump mwishoni wa mwezi Juni. Katika barua aliyoituma kupitia mitandao yake ya kijamii, Biden amesema imekuwa ni Fahari ya Maisha yake kuhudumu kama rais. "Na ingawa imekuwa nia yangu ya kutaka kuchaguliwa tena, naamini ni kwa manufaa ya chama changu na nchi kwa mimi kujiondoa na kuzingatia tu kutimiza wajibu wa Rais kwa kipindi kilichosalia cha muhula wangu". BBC News,  Swahi  nje.   Chanzo: bbc Swahili

Viongozi na Wanachama wa Klabu ya Yanga Tawi la Musoma Wamlilia Adam Gunje

Na Shomari Binda-Musoma UONGOZI wa timu ya Yanga tawi la Musoma umeelezea mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa kipindi kirefu wa aliyekuwa Mwenyekiti wa tawi hilo Marehemu Adam Said Gunje. Akimzungumzia kiongozi huyo wa zamani aliyeongoza tawi la Musoma na kiongozi wa mkoa wa Mara kwa zaidi ya miaka 30, Mwenyekiti wa sasa wa Yanga tawi la Musoma na mratibu wa mkoa wa Mara Ismail Massaro amesema moja ya jambo kubwa alilolifanya Gunje ni kuwaunganisha wana Yanga. Amesema kwa kipindi chote cha uongozi wake amekuwa karibu na wanachama na mashabiki wa Yanga Musoma na mkoa wa Mara na kupelekea kuwa na nguvu. Massaro amesema aliposhika nafasi hiyo alipewa ushirikiano wa karibu na Adam Gunje katika kuendelea kuwaunganisha wana Yanga. Amesema ili kuendelea kuweka kumbukumbu zake vizuri kwenye tawi la Musoma wataendelea kuiga mazuri yote aliyofanya ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha wana Yanga. " Ametangulia mbele ya haki mzee wetu lakini sisi kama Yanga tawi la Musoma tutaendelea kui...

Meli Vita Ya Matibabu Toka China Yahudumia Watu Zaidi ya 5000 Dar es Salaam

Melivita ya matibabu iitwayo 'Peace Ark' ya Jeshi la Ukombozi la watu wa China imetoa matibabu kwa wagonjwa zaidi ya elfu 5,000 kwa siku Tano baada ya kukita nanga katika bandari ya Dar Es Salaam nchini Tanzania Julai 16, 2024 itakayotoa huduma kwa siku Saba. Waziri wa Afya Mhe. @ummymwalimu amesema hayo leo Julai 21, 2024 baada ya kutembelea na kukagua utoaji wa huduma za Afya kwa wananchi pamoja na kujionea aina ya huduma zinazotolewa  na timu ya madaktari bingwa na bobezi wa meli ya Jeshi la Ukombozi (PLA) la Jamhuri ya Watu wa China. "Huduma zinazotolewa na wataalamu hawa wa  kichina wakishirikiana na wataalamu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ni pamoja na uchunguzi, matibabu ya aina zote za magonjwa ya nje, Magonjwa ya Upasuaji na Upasuaji wa kutumia Roboti, Magonjwa ya Mifupa, Uzazi na Magonjwa ya Kinamama, kutibu kwa kutumia Tiba Asili, Magonjwa ya njia ya Chakula pamoja na huduma za wagonjwa Mahututi (ICU). Amesema, Meli hii ilipanga kuona na kutoa hudum...

Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Awaagiza Wakurugenzi Kuandaa Maadhimisho ya Juma la Elimu

Na.Angela Sebastian  KATIBU tawala wa mkoa wa Kagera  Steven Ndaki  amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya mkoani humo kuhakikisha wanaanda maadhimisho ya juma la elimu maalum katika Maeneo yao ili kuwezesha wananchi kupata uelewa kwa yanayofanywa na idara hiyo. Hayo yamebainishwa katika taarifa iliyosomwa na katibu tawala msaidi idara ya uchumi na biasharea Isaya Tendega  kwa niaba ya katibu tawala,wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kwa maafisa elimu wa elimu maalum na wakuu wa shule zinazotoa elimu maalum mkoani humo yalifofanyika jana katika shule ya sekondari Omumwani . Amesema kuwa licha ya kwamba  mkoa utafanya maadhimisho ya juma hilo lakini pia kila Halmashauri lazima inatakiwa kufanya madhimisho katika maeneo yake lengo likiwa ni kuwezesha wananchi waudhulie na kupata elimu ya kutosha juu ya idara ya elimu maalum na watu wazima sambamba na majukumu yake na faida zake. “Tunatakiwa kuendelea kuadhimisha juma la elimu ya watu wazima kwa k...

Majaliwa: Wapiga Kura Wapya Zaidi ya Milioni 5 Kuandikishwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 jumla ya wapiga kura wapya 5,586,433 wataandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Amesema kuwa wapiga kura hao ni ambao watakuwa wametimiza umri wa miaka 18 katika kipindi cha kuanzia mwaka 2020 baada ya uchaguzi mkuu uliopita na ambao watatimiza umri huo ifikapo tarehe ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Amesema hayo leo (Jumamosi, Julai 20, 2024) alipozindua uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, katika uwanja wa Kawawa, mkoani Kigoma. Uzinduzi huo unaashiria kuanza kwa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura nchi nzima ambapo Mikoa inayoanza uboreshaji wa daftari hilo leo Julai 20, 2024 hadi  Julai 26, 2024 ni Kigoma, Katavi na Tabora kisha mikoa mingine kufuata. Ameongeza kuwa kwa mujibu wa taarifa za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, inakadiriwa kuwa wapiga kura 4,369,531 wataboresha taarifa zao. “Idadi hii si ndogo kwenye zoezi la uboreshaji wa daftari ...