Na.Angela Sebastian
KATIBU tawala wa mkoa wa Kagera Steven Ndaki amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya mkoani humo kuhakikisha wanaanda maadhimisho ya juma la elimu maalum katika Maeneo yao ili kuwezesha wananchi kupata uelewa kwa yanayofanywa na idara hiyo.
Hayo yamebainishwa katika taarifa iliyosomwa na katibu tawala msaidi idara ya uchumi na biasharea Isaya Tendega kwa niaba ya katibu tawala,wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kwa maafisa elimu wa elimu maalum na wakuu wa shule zinazotoa elimu maalum mkoani humo yalifofanyika jana katika shule ya sekondari Omumwani .
Amesema kuwa licha ya kwamba mkoa utafanya maadhimisho ya juma hilo lakini pia kila Halmashauri lazima inatakiwa kufanya madhimisho katika maeneo yake lengo likiwa ni kuwezesha wananchi waudhulie na kupata elimu ya kutosha juu ya idara ya elimu maalum na watu wazima sambamba na majukumu yake na faida zake.
“Tunatakiwa kuendelea kuadhimisha juma la elimu ya watu wazima kwa kila Halmashauri ili watu waweze kutambua dhana ya elimu ya watu wazima na nje ya mfumo rasmi hivyo naelekeza pamoja na kuwepo juma la elimu ya watu wazima kimkoa ni lazima kila Halmashauri ifanye maadhimisho yake, pamoja na kuendeleza kwa ufanisi dhana ya elimu jumuishi sawia na elimu ya watu wazima na ile nje ya mfumo rasmi ili watu waweze kutumia vituo au shule zilizopo kujiendeleza kielimu na kuondoa unyanyapaa kwa watoto wenye mahitaji maalum”ameeleza Tendega.
Kwa upande wake Afisa elimu watu wazima,elimu nje ya mfumo rasmi na elimu maalum mkoa wa Kagera Mwalimu Fortunatus Kahwa amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwapatia ujuzi wa kisasa walimumu hao kuhusu utendaji bora na kuandaa mkakati wa kufanikisha madhimisho ya elimu ya watu wazima mkoa wa Kagera ambayo yanatarajiwa kufanyika 13 hadi 16 mwezi Septemba katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe.
“Mafunzo haya pia yatawajenga na kuondolea kufanya kazi kwa mazoea na kupata takwimu sahii za kiutendaji katika Nyanja za kiutendaji katika elimu ya watu wazima na elimu maalum ambapo wataelewa namna ya utoaji wa elimu maalu na nje ya mfumo rasmi na kupata maelekezo mapya kutoka TAMISEMI”Ameeleza Kahwa.
Naye Afisa elimu taaluma mkoa wa Kagera mwalimu Simon Chiboni amesema wanawajengea uwezo walimu hao kwasababu katika uteuzi wao wapo baadhi walipata nafasi hizo bila kupata mafunzo hivyo ni maagizo ya TAMISEMI kuhakikisha wanapata mefunzo ili wote waweze kwenda sawa katika kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Aidha mkufunzi mkazisaidizi wa mkoa Kagera Charles Mkwidu amesema elimu ya watu wazima na nje ya mfumo rasmi inatoa fursa ya kipekee kupata ujuzi ambao mtu hakuwa nao au alikosa fursa ya kuupata katika waki na umri sahii kutokana na sababu mbalimbali bila kujali jinsi na umri ulio nao.



Comments
Post a Comment