Waziri Nyansaho afanya Mazungumzo na Ujumbe wa Kijeshi kutoka Algeria

GEORGE MARATO TV
0


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho (kulia pichani juu), jana Mei 11, 2026 alikutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Jeshi la Algeria ukiongozwa na Brigedia Jenerali Abbas Ibrahim.

Mazungumzo hayo ambayo yalifanyika kwenye ofisi ndogo za Wizara hiyo, Upanga jijini Dar es Salaaam, yalijikita katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Algeria katika masuala ya ulinzi, usalama na mafunzo ya kijeshi.

Brigedia Jenerali Abbas alitumia fursa hiyo kumfikishia Waziri Nyansaho salamu kutoka kwa Waziri wa Ulinzi wa Algeria na Rais wa Jamhuri ya Algeria, Abdelmadjid Tebboune, ambaye ameipongeza Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza amani na utulivu, na kuifanya nchi kuwa kisiwa cha amani.

Aidha, Brigedia Jenerali Abbas alimueleza Waziri Nyansaho kuwa nchi ya Algeria inajivunia mahusiano ya muda mrefu na kihistoria kati ya nchi hizo mbili.

Mazungumzo hayo kati ya Waziri Nyansaho na Ujumbe wa Jeshi la Jamhuri ya Algeria yalihudhuriwa pia na Balozi wa Algeria nchini Tanzania, maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top