Waziri Mkuu, Dkt Mwigulu Nchemba leo Machi 31, 2026 amewasili Iringa Mjini akiwa njiani kwenda Idodi kumuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mhe. William Lukuvi.
Kwenye uwanja wa Ndege wa Iringa, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu alipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James.




