waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Mheshimiwa Dkt Rhimo Nyansaho (mb), tarehe 19 January,2026 amekutana na kamati ya kudumu ya bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mambo ya nje, ulinzi na usalama maarufu ikijulikana kama NUU katika ofisi za Bunge jijini Dodoma kwa ajili ya kuwasilisha taarifa ya wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga Taifa
Kikao hicho kati ya waziri wa ulinzi na JKT na kamati ya kudumu ya bunge inayoongozwa na mwenyekiti wake, Mheshimiwa Najma Murtaza Giza na makamu mwenyekiti wake Mheshimiwa Pascal Inyasi Chinyele ilihusisha kamati hiyo ya Bunge kupewa taarifa ya majukumu na muundo wa wizara ya ulinzi na JKT inayoongozwa na Mhe.Dkt.Rhimo Nyansaho aliyeteuliwa Tarehe 17 Novemba 2025 na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa.






