Skip to main content

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Biteko Anadi Fursa Za Uwekezaji Sekta ya Nishati Kimataifa


📌 Dkt. Samia achagiza mapinduzi ya nishati Afrika

📌 Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia yajadiliwa kimataifa


Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewakaribisha wawekezaji kutoka nchi mbalimbali duniani kuwekeza katika sekta ya nishati nchini.

Akizungumza leo Februari 12, 2025  jijini New Delhi, India katika Mkutano wa Mawaziri wa Nishati kutoka India, Sudan, Malawi, Rwanda, Nepal, Brazili pamoja na wakurugenzi wa kampuni mbalimbali kutoka India Dkt. Biteko amesema Serikali imeweka mazingira wezeshi ili kuhakikisha  Nishati Safi ya Kupikia inapatikana kwa urahisi na gharama nafuu.

 Mwaka 2022 Serikali ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ilisisitiza matumizi ya nishati safi na kueleza athari za matumizi ya nishati isiyokuwa safi kwa kuanzisha mjadala wa kwanza kuhusu matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia na faida zake kiuchimi na Kijamii.

Dkt. Biteko  ametaja fursa mbalimbali za biashara ya Nishati Safi ya Kupikia nchini Tanzania, kama vile ujenzi wa miundombinu ya uzalishaji, kupokea, kuhifadhi na kusambaza nishati safi ya kupikia

Fursa zingine ni vituo vya kupokea LPG, vifaa vya uhifadhi, miundombinu ya usambazaji wa gesi asilia katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam na maeneo jirani, usambazaji wa LNG wa kiwango kidogo, vifaa na mitungi ya gesi asilia.

“ Ningependa kuchukua fursa hii kuwataka wadau wote na wawekezaji katika sekta ya nishati kujiunga nasi katika malengo yetu makubwa lakini yanayoweza kufikiwa ya kupata umeme na nishati safi ya kupikia kuongeza sehemu ya nishati mbadala katika mchanganyiko wa nishati na kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi ili kusaidia upatikaji wa nishati,” amesema Dkt. Biteko.

ametaja jitihada za Serikali za kuhamasisha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia “Tanzania imekamilisha maendeleo ya Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa mwaka 2024-2034 wenye lengo kuu la kuhakikisha kuwa asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034, ”

Ameongeza kuwa uzoefu unaonesha kuwa “ Katika kujifunza India imefanya vizuri  katika matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia na takwimu zinaonesha kwamba  mwaka 2023, asilimia 71.1 ya watu wa India walikuwa wakitumia nishati safi ya kupikia. Hii imetokana na umuhimu wa kuhusisha sekta binafsi na kuunganishwa kwa ruzuku kwa kaya zenye kipato cha chini,” amesema Dkt. Biteko.

Dkt. Biteko amesema takriban watu bilioni 2.3 duniani hawapati nishati safi ya kupikia na watu milioni 990 Kusini mwa Jangwa la Sahara hawajafikiwa matumizi na nishati safi. Hali hii inasababisha matatizo ya afya, uharibufu wa mazingira na matatizo ya kiuchumi,”


Vilevile, amesema Rais Samia amedhamiria kuinadi ajenda ya nishati safi ya kupikia nje ya mipaka ya Tanzania na Afrika, ambapo katika mkutano wa COP 28, alizindua Programu ya Uwezeshaji wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Wanawake wa Afrika (AWCCSP), iliyoelekezwa kukabiliana na changamoto kubwa za kijinsia, mazingira, afya, na kiuchumi zinazowakabili wanawake na wasichana barani humo.


Akiendelea kuelezea msimamo wa Tanzania katika kuhamasisha Ajenda ya Matumizi ya Nishati Safi kimataifa, Dkt Biteko amesema mwaka 2024 Rais Samia alishiriki katika Mkutano wa Juu wa Nishati  Safi ya Kupikia  nchini Ufaransa ambapo alikuwa Mwenyekiti mwenza, na takriban dola bilioni 2.2 ziliahidiwa kwa  ajili kusaidia ajenda hiyo barani Afrika.


Aidha, Tanzania kwa kushirikiana na Tume ya Nishati ya Afrika (AFREC) ilifanya Mkutano wa Kiwango cha Juu kuhusu Kupikia Safi barani Afrika katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mnamo Septemba 2024 pamoja na kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika uliyofanyika jijini Dar es salaam Februari  27 na 28 mwaka huu kwa ajili ya kueleza dhamira zao kuhusu Mikataba ya Nishati ya Kitaifa.

Kwa upande wake, Waziri wa Petroli na Gesi Asilia wa India, Mhe. Hardeep Singh ametaja madhara ya matumizi ya nishati isiyosafi  “ Kumekuwepo na idadi ya vifo takribani milioni 2, lakini wanawake na watoto wanapata madhara zaidi, huku wanawake wakitumia hadi saa 5 kila siku kwa ajili ya kutafuta kuni na kuandaa chakula,”

Akielezea mafanikio ya matumizi ya nishati safi nchini India, amesema sasa watu milioni 330 wameunganishwa na matumizi ya gesi au nishati safi.

“ Nishati safi sasa inapatikana kwa watu na maisha yamekuwa rahisi na shughuli zimeendelea kufanyika kwa ufanisi, sioni kwa nini hatuwezi kufanya hivi kwa kila mwananchi  inawezekana.” Amemalizia Mhe. Signh

Kimsingi mkutano huo wa Mawaziri wa Nishati unatajwa kuwa muhimu katika jitihada za kuendeleza matumizi ya nishati safi duniani ambao umetoa fursa kwa mawaziri waliohudhuria kueleza jitihada zinazofanyika za kukuza matumizi ya nishati safi katika nchi zao.

Aidha, masuala ya sera, mila za watu, uhamasishaji, ubunifu, miundombinu ya usambazaji na wawekezaji yanatajwa kuwa mchango muhimu ya mafanikio ya matumizi ya nishati safi.



Comments

#maratotv

RAIS RUTTO AAMBATANA NA ODINGA NCHINI CHINA

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh William Rutto na mke wake wamewasili nchini China kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC). Katika ziara hiyo ameambatana na waziri mkuu mstaafu wa nchi hiyo Raila Odinga ambaye pia anapigiwa kampeni ili aweze kushinda nafasi ya Uenyekiti wa AU.

WIZARA YA MALI ASILI YASISITIZA MATUMIZI YA SHERIA NA KANUNI KATIKA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA UHIFADHI

Na.Joyce Ndunguru, Morogoro. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii anaeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba asisitiza matumizi ya sheria na kanuni katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za uhifadhi. Kamishna Wakulyamba ameyasema hayo leo Septemba 1, 2024 wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya katika ofisi za Makao Makuu ya TAWA yaliyopo Mkoani Morogoro kwa lengo la kuongea na watumishi ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kukagua maeneo ya kazi. "Kama wahifadhi tunapaswa kufahamu sheria zote zinazosimamia masuala ya uhifadhi zilizopo katika Taasisi zetu pamoja na za Taasisi zingine za uhifadhi zilizopo ndani ya Wizara ya Maliasili na utalii" amesema Kamishna Wakulyamba. "Pamoja na kufahamu sheria na kanuni zilizopo ndani ya Wizara yetu, ni vyema kufahamu na kuzingatia sheria nyingine za Nchi ambazo zinatuzunguka ili ziweze kutusaidia katika utekelezaji wa majukumu yetu mfano sheria inayohusiana na ukusanyaji wa vielelezo kuanzia kw...

Rais Dkt. Samia Awasili China Kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano Kati ya China na Africa FOCAC

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing Capital nchini China kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) tarehe 03 Septemba, 2024.

MAKOMANDOO MIAKA 60 YA JWTZ,HAIJAWAHI KUTOKEA

Makomandoo ya jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ)wamekuwa kivutio cha aina yake kwenye kikele cha maadhimisho ya miaka 60 ya tangu kuanzishwa kwa jeshi hilo. Katika sherehe hizo ambazo zimefanyika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshiriki kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika uwanja huo wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, leo tarehe 1 Septemba, 2024. Rais ameonesha kujivunia na kulipongeza JWTZ kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya kuanzishwa kwake huku akitumia nafasi hiyo kuwapongeza Marais waliomtangulia kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wa uongozi wao kwa kuliongoza vema jeshi hilo.

Meli ya Mv. Serengeti yapinduka na kuzama katika Bandari ya Mwanza kusini

 Meli Mv.Serengeti imepinduka na kuzama kwenye bandari ya mwanza kusini.  Meli hiyo imepinduka na kuzama disemba 26 majira ya saa Saba za usiku.  Tukio hilo limetokea meli hiyo ikiwa imefungwa katika gati la bandari ya mwanza kusini.  Kampuni ya meli Tanzania(Tashico) imethibitisha meli ya Mv. Serengeti kupinduka na kuzama upande mmoja wa nyuma.  Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma cha Kampuni hiyo inaeleza kuwa Tashico imeshirikiana na Timu mbalimbali za Wataalam kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa bandari (TPA) na wadau wengine katika Juhudi za Uokoaji.  Kwa Mujibu wa Taarifa hiyo,Taarifa rasmi ya chanzo cha Tatizo itatolewa Meli hiyo itakapokuwa imeinuliwa na Uchunguzi wa kubaini Tatizo utakapokuwa umefanyika. Meli ya Mv.Serengeti inadaiwa kusitisha safari zake kwenye ziwa Victoria mwaka 2016  Meli ya Mv.Serengeti imepinduka na kuzama katika...

Jenerali Jacob Mkunda Atembelea Meli Tiba ya China Aridhishwa na Huduma

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda ametembelea meli tiba ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Peace Ark ili kuona matibabu yanavyofanyika. Jenerali Mkunda amefurahishwa na namna wataalam wa tiba wa Jeshi la China walivyotoa matibabu kwa kushirikiana na wataalam wa tiba wa JWTZ . Meli tiba ya jeshi la China imekuja hapa nchini na kutia nanga kwenye bandari ya Dar Es Salaam kutoa matibabu mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa JWTZ  na ushirikiano wa miaka 60 baina ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la Watu wa  China. Matibabu hayo yalianza kutolewa tarehe 18 Julai 2024 hadi tarehe 22 Julai 2024. Meli tiba hiyo itaondoka hapa nchini tarehe 23 Julai mwaka huu.

AMIRI JESHI MKUU AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 60 YA JWTZ

 Mapema leo asubuhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride Maalumu la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Uwanja wa Uhuru leo September 01,2024. Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa jeshi la ulinzi la Wananchi Tanzania si jeshi la Uvamizi bali ni jeshi la ulinzi wa Wananchi Tanzania Amewahakikishia wanajeshi kufanya kazi kifua mbele,kuwa amiri jeshi mkuu yuko pamoja nao wakati wote.

Mbunge wa Bukoba Vijijini ameaga Sifa Kedekede Kwa Rais Samia

 Na Angela Sebastian; Bukoba  MBUNGE wa jimbo la Bukoba vijijini Dk. Jasson Rweikiza amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo, kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ambayo ni lango la kutoka na kuingia ndani ya mkoa wa Kagera. Ametoa shukrani hizo wakati akiongea wananchi mbalimbali waliofika katika viwanja vya Rweikiza pre and Primary school iliyoko eneo la Kyetema Bukoba vijijini, kwa kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa baba wa mbunge huyo aliyekuwa akiitwa Samsoni Rweikiza.  Rweikiza amebainisha kuwa,Dk. Samia Suluhu Hassan ni Rais mwenye upendo amekubali kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya Bukoba Vijijini na ndiyo maana tunasema atakuwa kiongozi wetu kwa awamu nyingine tena,tunapaswa kila mmoja kumuunga mkono. ametaja madaraja hayo kuwa ni Karebe ambalo limetengewa kiasi cha shilingi bil.9.3 kwa ajili ya ukarabati mkubwa kutokana na daraja ...

Jenerali ameacha alama ya uzalendo na kujitoa kwa ajili ya Taifa

*📌 Serikali itaenzi na kuthamini mchango wake* *📌 Asema Jenerali Musuguri alijitolea kuhakikisha Tanzania inabaki na amani na usalama* *📌 Asema alikuwa mstari wa mbele kuliokoa Taifa* *📌 Aiasa jamii kuacha alama katika maisha ya kila siku* *📌 Dkt. Biteko aongoza mamia ya watu mazishi ya Jenerali Musuguri Butiama* Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa  aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Mstaafu David Bugozi Musuguri alijitolea  kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa na amani, usalama na mshikamano pamoja na kuifundisha jamii  moyo wa dhati wa kuilinda nchi. Dkt. Biteko amesema hayo leo Novemba 4, 2024 Butiama mkoani Mara wakati akiwasilisha salamu za Serikali kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Jenerali Mstaafu Musuguri. “ Katika  uhai wa kila mmoja wetu ni jambo gani mtu atakumbukwa nalo, baba huyu a...

Majaliwa Achangisha Shilingi Milioni 900 za Ujenzi wa Kanisa Kuu Lindi

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameendesha harambee na kuchangisha sh. milioni 928.67  za ujenzi wa kanisa kuu tarajiwa la Mt. Andrea Kagwa la Jimbo Katoliki la Lindi. Kati ya fedha hizo, sh. milioni 464.3 ni fedha taslimu na nyingine kati ya hizo zimeshawekwa benki na sh. milioni 464.37 bado ni ahadi. Awamu ya kwanza ya ujenzi huo, inatarajiwa kugharimu sh. milioni 700. Akizungumza na waumini na wadau mbalimbali waliohudhuria harambee iliyofanyika Ruangwa mjini, leo mchana (Jumamosi, Julai 27, 2024), Waziri Mkuu amewataka waliotoa ahadi wazikamilishe mapema ili kazi ya ujenzi isikwame. "Ninawashukuru sana wote mliofika na wote waliochangia ujenzi wa kanisa tarajiwa. Ninawaomba walioahidi, wakamilishe ahadi zao mapema ili kazi ianze kwani ramani ipo, mafundi wapo tayari,  wasimamizi wa ujenzi wapo," amesisitiza.  Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, Mhashamu Askofu Wolfgang Pisa kuanza ujenzi wa kanisa kuu la jimbo hilo, ni utekelezaji ...