Waziri Mkuu Kuzindua Taarifa za Maboresho ya Mazingira ya Uwekezaji na Biashara

GEORGE MARATO TV
0



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 11, 2024 atazindua Taarifa za Maboresho ya Mazingira ya Uwekezaji na Biashara pamoja na  Nyenzo za Usimamizi wa Uwekezaji, katika Ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, Jijini Dar es salaam. 

Taarifa na nyenzo hizo zitasaidia  katika kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kwa kutoa mwongozo, kuboresha taratibu na kuongeza ufanisi. 

Aidha, Nyenzo hizo zitasaidia katika kupima maendeleo, kutatua changamoto na kuhakikisha kwamba uwekezaji unakua katika mazingira rafiki na yenye ushindani.

Viongozi wengine wanaoshiriki katika tukio hilo ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Stanslaus Nyongo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top