Mbunge Agnes Mathew Marwa Achangia Mbao 415 Kwa Ajili ya Kuezeka Nyumba ya Katibu wa UWT Musoma Mjini

GEORGE MARATO TV
0



MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Mara Mhe. Agnes Mathew Marwa amechangia mbao 415 kwa ajili ya kuezeka nyumba ya Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM ( UWT ) Musoma mjini iliyoanza kujengwa toka 2023.

Mhe. Agnes Mathew amekabidhi mbao hizo wakati wa sherehe ya maadhimisho ya wiki ya Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) iliyofanyika Septemba 16 Kamnyonge manispaa ya Musoma.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mbao hizo kwa niaba ya Mhe. Agness Mathew diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Musoma amesema katika ametoa mchango huo ili kuweza kukamilisha nyumba hiyo ili kumuwezesha katibu kutekeleza majukumu ya Jumuiya na Chama kwa ufanisi..

Stella Mtani ni mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Musoma akizungumza katika madhimisho ya sherehe hizo amesema nyumba hiyo ya katibu ilianza kujengwa tangu mwaka 2023 na wamekua wakipokea vifaa kutoka kwa viongozi mbalimbali huku akieleza kuwa Mhe. Agness mbali na kuchangia mbao hizo 415 lakini pia aliwahi kuchangia mifuko 40 ya sementi wakati jengo hilo lilipoanza kujengwa.

Spelazia Mgita mkazi wa makoko manispaa ya Musoma ni miongoni mwa wanawake walioshiriki maadhimisho hayo ambaye mbali na kumpongeza Mhe. Agnes lakini pia amemshukuru  kwa mchango wake anaotoa kwa ajili kukamilisha ujenzi huo.

Kwa upande wake Katibu wa UWT mkoa wa Mara Zaidan Mwamba ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo akizungumza mara baada ya kupokea mbao hizo amemshukuru Mhe. Agnes kuwa mstari wa mbele katika kujitoa kuchangia Jumuiya katika maswala mbalimbali ya maendeleo.

Viongozi mbalimbali wamechangia vifaa katika maadhimisho hayo ya wiki ya UWT  huku pia sherehe za maadhimisho hayo zikiambatana zoezi la kupanda miti kwenye eneo la ujenzi wa nyumba ya Katibu iliyopo kamnyonge manispaa ya Musoma.







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top