Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Serikali yakutana na Mjumbe Malaam wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola

Na, Mwandishi Wetu Ujumbe wa Serikali ya Tanzania ukingozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi, imekutana na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola na Rais wa zamani wa Malawi, Mhe. Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera, na kujadiliana kuhusu namna Tanzania ilivyojidhatiti katika kudumisha umoja, amani na mshikamano miongoni mwa Watanzania. Kikao hicho kilifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) siku ya Alhamisi Aprili 9, 2026 mchana baada ya Mheshimiwa Chakwera kumtembelea Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahamoud Thabit Kombo, ikiwa ni ishara ya kuanza rasmi kwa ziara ya Mjumbe huyo Maalum nchini Tanzania. Katika kikao hicho, Mhe. Profesa Kabudi alimueleza kwa kina Mjumbe huyo Maalum, kuhusu hatua mbalimbali zinazoendelea kuchululiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kuimarisha demokrasia nchin...

Kamati ya Bunge Yajengewa Uwezo Kuhusu Programu ya Afdp

NA, MWANDISHI WETU - DODOMA Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, chini ya Makamu Mwenyekiti wake Mheshimiwa Edwin Swalle, imejengewa uelewa kuhusu utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inayoratibiwa na kusimamiwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu na kuipongeza Ofisi hiyo kwa namna inavyoratibu na kuhakikisha Programu inayafikia malengo kwa tija ya Taifa kwa ujumla. Akizungumza baada ya semina fupi iliyoandaliwa na Ofisi hiyo, Mheshimiwa Swalle amesema mradi wa AFDP umefanikiwa kuwafikia wananchi wengi kupitia ukuzalishaji wa mbegu bora za Kilimo, kilimo cha zao la mwani na uzalishaji wa vifaranga vya samaki, hatua inayochochea maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi. Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuwashirikisha Wakurugenzi wa Halmashauri ili kubaini mahitaji halisi ya wananchi na kuhakikisha mradi huo unawanufaisha watu wengi zaidi na kuendelea kuwa na tija kwa jamii. Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mku...

Doris Mollel umestahili tuzo ya WHO, umeokoa maisha ya wengi

Na: Dk. Reubeni Lumbagala Nakumbuka mwalimu wangu wa somo la Uraia (Civics) alipokuwa akitufundisha mada (topic) ya "Haki za "Binadamu" (Human Rights) tulipokuwa Kidato cha Kwanza, alituambia mengi kuhusu haki za binadamu.  Miongoni mwa mikazo yake, alituambia hivi: Haki ya kuishi (Right to life) ndiyo haki kubwa kuliko zote maana mtu anapokuwa hai ndipo anakuwa na uwezo wa kupata haki nyingine zote. Nilimwelewa vizuri sana. Kimsingi, uhai ni muhimu katika maisha ya mwanadamu, ndiyo maana inapotokea mtu ameugua, na akawa hana uwezo wa kumudu gharama za matibabu yake, basi familia, ndugu, jamaa na marafiki hushikamana kwa kuchangishana fedha kunusuru uhai wa ndugu yao huyo. Watoto ni kundi ambalo lipo hatarini kukabiliwa na magonjwa mbalimbali. Ni kutokana na msingi huo, serikali inajitahidi sana kutoa chanjo za magonjwa mbalimbali ili kuimarisha na kujenga afya zao ili kuwa na kinga ya kutosha ya kuweza kupambana na magonjwa. Taasisi ya Doris Mollel (DMF) ni wadau muhimu...

Tanzania: CRJE and Asiano Global Sign Tsh48 Billion Deal to Implement Keyne Center Project in Dar

By Prosper Makene  In a major boost to Tanzania's construction sector, CRJE (East Africa) Ltd and Asiano Global Investment Company Limited have signed a whopping Tsh48 billion deal to build a 26-floor project in Dar es Salaam. The project which is expected to be a game-changer in the city's skyline and will be completed in June 2028. The project is part of Tanzania's Vision 2050, which aims to support the government which has identified infrastructure development as a key priority, and projects like this are expected to play a major role in achieving this goal. The 26-floor project will be located in the heart of Dar es Salaam, providing easy access to key business and social amenities. The project will include commercial spaces, residential apartments, and modern amenities, making it a unique blend of business and luxury living. The project is also a part of a larger trend of investment in Tanzania's construction sector. The government has launched several initiatives ...

Tanzania: CRJE na Asiano Global Saini Makubaliano ya Shilingi Bilioni 48 Kutekeleza Mradi wa Kituo cha Keyne jijini Dar

Na Prosper Makene  Katika kuimarisha sekta ya ujenzi nchini Tanzania, CRJE (East Africa) Ltd na Asiano Global Investment Company Limited wamesaini mkataba wa thamani ya shilingi bilioni 48 wa kujenga mradi wa ghorofa 26 jijini Dar es Salaam. Mradi huo unatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika anga ya jiji na utakamilika Juni 2028. Mradi huu ni sehemu ya Dira ya Tanzania ya 2050, ambayo inalenga kuunga mkono serikali ambayo imetambua maendeleo ya miundombinu kama kipaumbele muhimu, na miradi kama hii inatarajiwa kuchukua jukumu kubwa katika kufikia lengo hili. Mradi huo wa ghorofa 26 utakuwa katikati ya jiji la Dar es Salaam, ukiwapa ufikiaji rahisi wa huduma muhimu za biashara na kijamii. Mradi huo utajumuisha maeneo ya kibiashara, vyumba vya makazi, na huduma za kisasa, na kuufanya kuwa mchanganyiko wa kipekee wa biashara na maisha ya anasa. Mradi huu pia ni sehemu ya mwelekeo mkubwa wa uwekezaji katika sekta ya ujenzi nchini Tanzania. Serikali imezindua mipango kadhaa ya kuvut...

Watendaji Ofisi ya Waziri Mkuu Wakumbushwa Kuimarisha Weledi Kutimiza Dira ya Taifa 2050

Na. MWANDISHI WETU -DODOMA Watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu wamekumbushwa kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi, ufanisi na kujituma ili kuhakikisha wanachangia kikamilifu katika kufanikisha malengo ya Dira ya Taifa 2050, hususan katika maeneo ya sera, uratibu na usimamizi wa utekelezaji wake. Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mhe. Prof. Palamagamba J.A. Kabudi, wakati akizungumza na watumishi wa Ofisi hiyo mara baada ya kuwasili rasmi na kupokelewa na uongozi na watumjshi wa Ofisi hiyo katika Jengo la Ngome Jijini Dodoma tarehe 8 Machi, 2026 Prof. Kabudi alisisitiza umuhimu wa ushirikiano na ubunifu miongoni mwa watumishi ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi. “Ni muhimu tushirikishane mawazo na kufanya kazi kwa pamoja ili kumsaidia Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufanikisha adhima ya maendeleo yenye kuleta ustawi na furaha kwa Watanzania," alisema Prof. Kabudi Aliongezea kuwa upo umuhimu wa kus...