WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa barabara ya Kagwira – Karema (kilometa 112) katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi. Mradi huo unatekelezwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa gharama ya takribani shilingi bilioni 219.09, ukiwa na lengo la kuboresha miundombinu ya usafiri na kuchochea shughuli za kiuchumi katika ukanda wa Ziwa Tanganyika. Kwa mujibu wa taarifa ya mradi iliyosomwa na Kaimu Meneja wa Udhibiti wa Miradi TANROADS, Mhandisi Malima Musema Mongo, ujenzi wa barabara hiyo umegawanyika katika vipande viwili ambavyo ni Kagwira – Kasekese (kilometa 54.144) na Kasekese – Ikola – Karema (kilometa 56.911). Alisema ujenzi wa kipande cha Kagwira – Kasekese unagharimu takribani shilingi bilioni 106.95 na umefikia asilimia 8.2 ya utekelezaji, huku kipande cha Kasekese – Ikola – Karema kikigharimu takribani shilingi bilioni 112.14 na kufikia asilimia 33.4 ya utekelezaji. Mradi huo ni wa kimkakati kwa kuwa utarahisi...
Marato tv - Sauti ya Jamii