- Ajira 122 zatengenezwa, Serikali yavuna Shilingi Milioni 400/- 📍Rombo, Februari 28, 2026 MGODI wa Rock Block uliopo Wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro, umeendelea kuwa kichocheo cha mageuzi katika Sekta ya Madini ya Ujenzi kwa kuzalisha ajira 122 na kuiingizia Serikali zaidi ya Shilingi milioni 400 katika kipindi cha miaka mitatu ya uendeshaji wake. Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Abel Madaha, amesema hayo kupitia mahojiano maalum Wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro na kuongeza kuwa uchimbaji na uchongaji wa miamba kwa ajili ya kutengeneza matofali na bidhaa nyingine za ujenzi ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kusimamia na kuendeleza madini ya ujenzi ili kuongeza thamani na mapato ya taifa. Amesema mgodi huo umeendelea kuchangia mapato ya Serikali kupitia ada, mrabaha na kodi mbalimbali zinazolipwa kwa taasisi ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na Halmashauri ya Wilaya, hali inayochochea maendeleo ya kiuchumi katika eneo la Rombo na mkoa ...
Marato tv - Sauti ya Jamii