WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Februari 28, 2026 anaungana na waombolezaji kushiriki Adhimisho la Misa Takatifu ya Mazishi ya Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Marehemu Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo inayofanyika katika Kanisa la Hija ya Bikira Maria - Pugu Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi anaongoza waombolezaji katika mazishi.




