Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Wafanyabiashara Msiwaumize Wananchi-Dkt. Mwigulu

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka wafanyabiashara nchini kutowaumiza Watanzania kwa kupandisha bei za bidhaa hususani kipindi hiki cha kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na mfungo wa Kwaresma kwa kuwa nchi kwa sasa haina upungufu wa chakula. Amesema licha ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) nchini kutangaza kuwepo kwa upungufu wa mvua katika maeneo mengi nchini lakini nchi inautoshelevu wa chakula hivyo hakuna sababu ya kupandisha bei za vyakula. Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi, Januari 29, wakati akijibu swali la Nancy Nyalusi, Mbunge wa Viti Maalum katika kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu. Mbunge huyo alitaka kujua Serikali imejipangaje kuhakikisha nchi inakuwa na utoshelevu wa chakula na kuzuia mfumuko wa bei kuelekea kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Kwaresma.   “…Kwa sasa tunachakula cha kutosha, mahitaji ya chakula cha akiba kwa nchi ni takribani tani 150,000 na sasa nchi ina zaidi ya tani 400,000 za akiba ya chakula rai ambay...

Serikali:Kila Mwananchi Mwenye Uhalali wa Kumiliki Ardhi, Apate Hati Yake

Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewahakikishia wananchi kuwa itahakikisha inasimamia Kila mwananchi mwenye uhalali wa kupata hati miliki ya ardhi ya eneo lake analomiliki. Akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye Kliniki Maalum ya Ardhi inayoendelea katika Ofisi za Ardhi Mkoa wa Dodoma Naibu waziri Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi  Mhe. Kaspar Mmuya amesema, upo umuhimu wa kuhakikisha wananchi waliokamilisha taratibu za kumilikishwa wanapata hati zao kwa Kwa wakati. "Nitasimama kuhakikisha kila mwananchi mwenye uhalali wa kumiliki Ardhi anapata hati yake kwa wakati” .amesema Naibu Waziri Mmuya. Sambamba na hayo Naibu waziri Mmuya amewataka wataalamu wa Sekta ya Ardhi nchini kuhakikisha wanatoa elimu ya matumizi bora ya ardhi pamoja na jinsi ya kupata hatimiliki za ardhi jambo litakalosaidia kuepusha ujenzi holela  unaoenda kinyume na matumizi yaliyopangwa. "Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kusimamia haki ya umiliki wa ardhi...

Dkt. Mwigulu Aongoza Mkutano wa Kamati ya Katiba, Sheria na Bunge

  Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo January 28,2026 ameongoza Mkutano wa Kamati ya Katiba, Sheria na Bunge ya Baraza la Mawaziri  kwenye ukumbi wa Spika, bungeni jijini Dodoma, Januari 28, 2026.

Dkt. Mwigulu Akutana na Frederick Sumaye

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 28, 2026 amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ofisini kwa Waziri Mkuu Mlimwa jijini Dodoma.

Waziri Kijaji Ampokea Braydon Bent

📍Atimiza ndoto yake ya siku nyingi ya kuitembelea Tanzania  Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amempokea shabiki mashuhuri wa klabu ya Manchester City ya Uingereza Braydon Bent ambaye ametimiza ndoto yake ya siku nyingi ya kuitembelea Tanzania na kujionea vivutio mbalimbali ikiwemo Serengeti na Mlima Kilimanjaro.  Ni kama safari iliyochukua karne hivi ya kutoka  tu Etihad Stdium hadi Serengeti! Shabiki huyo mtopezi wa Manchester City anasifika kwa kurekodi video akiongea Kiswahili na alipata kuahidiwa kuja Tanzania tangu mwaka 2020.  Leo, hatimaye, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi wametimiza ndoto ya shabiki huyo ambaye amepata pia kuwahoji mastaa kama Neymar, Aguero, Kocha Pep Guadiola na sasa akiwa mtangazaji wa mechi za Man City na pia akiwa na vipindi Sky News.  “Ilikuwa ndoto yangu kubwa kufika nchi hii nzuri. Kwa mapokezi haya naona kabisa tayari safari yangu imeanza ...

NIRC Yaimarisha Utunzaji wa Mazingira Kupitia Upandaji Miti Skimu ya Hombolo

📍 Hombolo, Dodoma KATIKA kuadhimisha siku ya kumbukizi ya kuzaliwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan,rai imetolewa kwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), kuendelea kutoa elimu kwa wakulima na jamii kuhusu umuhimu wa uhifadhi wa mazingira. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ametoa wito huo ameutoa leo Aprili 27, mkoani Dodoma wakati wa zoezi la upandaji miti katika Skimu ya Umwagiliaji Hombolo, lililoendeshwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji. Senyamule amesisitiza matumizi endelevu ya rasilimali za maji, na usimamizi shirikishi wa miundombinu ya umwagiliaji, ili kuongeza ufanisi na uimara wa miradi hii. "Serikali ya Mkoa wa Dodoma itaendelea kushirikiana kwa karibu na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji pamoja na wadau wote wa maendeleo katika kuhakikisha kuwa miradi ya umwagiliaji inatekelezwa kwa kuzingatia sheria, kanuni na misingi bora ya uhifadhi wa mazingira, sambamba na kukuza uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla. Senyamule amewahimiza wananchi wote kushiriki kikamilifu kat...