Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewahakikishia wananchi kuwa itahakikisha inasimamia Kila mwananchi mwenye uhalali wa kupata hati miliki ya ardhi ya eneo lake analomiliki.
Akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye Kliniki Maalum ya Ardhi inayoendelea katika Ofisi za Ardhi Mkoa wa Dodoma Naibu waziri Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Kaspar Mmuya amesema, upo umuhimu wa kuhakikisha wananchi waliokamilisha taratibu za kumilikishwa wanapata hati zao kwa Kwa wakati.
"Nitasimama kuhakikisha kila mwananchi mwenye uhalali wa kumiliki Ardhi anapata hati yake kwa wakati” .amesema Naibu Waziri Mmuya.
Sambamba na hayo Naibu waziri Mmuya amewataka wataalamu wa Sekta ya Ardhi nchini kuhakikisha wanatoa elimu ya matumizi bora ya ardhi pamoja na jinsi ya kupata hatimiliki za ardhi jambo litakalosaidia kuepusha ujenzi holela unaoenda kinyume na matumizi yaliyopangwa.
"Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kusimamia haki ya umiliki wa ardhi kwa vitendo na kuhakikisha wamiliki wa ardhi wanapata hati zao". Amesema Mmuya
"Huduma hii ni nchi nzima na Wananchi wataendelea kupata huduma za hati katika maeneo mbalimbali nchini". Ameongeza
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga amesema, wamiliki wa ardhi waliokamilisha taratibu za umiliki wapewe Hatimiliki zao na hawahitaji maneno mengi.
"Ni marufuku kwa mtumishi wa sekta ya ardhi anayefuatwa na mwanachi mwenye shida kumwambia aende kwa mtu mwingine kupata huduma na hili nitahakikisha kulisimamia Kwa ukaribu zaidi kwa kuwa mwananchi anachohitaji ni huduma". Amesisitiza
Zoezi la Kliniki Maalum ya Ardhi ambayo imejikita kutoa Hatimiliki za Ardhi katika jiji la Dodoma ni la siku 14 kuanzia 28 Januari hadi Februari 10, 2026.












Comments
Post a Comment