Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Dkt. Mwigulu Akagua Maendeleo ya Ujenzi wa Madaraja Lindi

_Asisitiza Rais Dkt. Samia amedhamiria kushughulika kwa vitendo na umasikini wa watanzania_ WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 19, 2025 amekagua maendeleo ya ujenzi wa Madaraja na Ukarabati wa barabara kuu ya Marendego-Nangurukuru-Lindi-Mingoyo Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amewaambia wakazi wa Somanga mkoani Lindi kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatekeleza miradi ya kimkakati ili kushughulika kwa vitendo na umasikini wa Watanzania.  Amesema kuwa Rais Dkt. Samia alisimamia ukamilishaji wa Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere ili kuhakikisha kila mtanzania ananufaika na huduma ya nishati ya umeme.  “Tumeshuhudia Rais Dkt. Samia namna anavyotekeleza miradi kwenye sekta mbalimbali ikiwemo uvuvi, maji, kilimo, afya, elimu na hata uwezeshaji wananchi kiuchumi”

Balozi Matinyi aongoza watanzania katika kikao muhimu nchini Uswidi

Balozi wa Tanzania nchini Uswidi, Mhe. Mobhare Matinyi (wa nne kutoka kushoto mstari wa mbele), akiwa pamoja na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Raddy Energy ya Tanzania, Ramadhani Mlanzi (kulia kwake), katika picha ya pamoja na wawakilishi wa taasisi za fedha za Serikali ya Uswidi, kampuni ya Siemens Energy, Benki ya CRDB, Ubalozi na Raddy Energy, jijini Stockholm, mara baada ya kikao kilichofanyika siku chache zilizopita kukamilisha mchakato wa ununuzi wa mitambo minne ya kuzalisha umeme wa gesi itakayoletwa nchini ili kuimarisha uzalishaji wa umeme nchini. Kikao cha pamoja baina ya Ubalozi wa Tanzania nchini Uswidi, kampuni ya Raddy Energy, Benki ya CRDB na wawakilishi wa taasisi za fedha za Serikali ya Uswidi wakiendelea na kikao jijini Stockholm, hivi karibuni.

Mkoa wa Tanga una ziada ya tani milioni moja ya chakula

    Na MASHAKA MHANDO, Tanga MKOA wa Tanga unaendelea kuimarika katika usalama wa chakula baada ya kurekodi ziada ya zaidi ya milioni moja, huku Mkuu wa Mkoa huo, Balozi Dkt. Batilda Burian, akiwataka wananchi na viongozi kuchukua hatua madhubuti udhibiti mfumo wa bei na matangazo wa mazao. Akizungumza katika mahojiano maalum jana chakula agizo la hivi karibuni la Serikali kuhusu mamlaka ya akiba ya nchini, Dkt. Batilda alisema kuwa licha ya kosa la idadi ya watu, mkoa unajitosheleza kwa wastani wa tani 668,776 za chakula kikavu kwa mwaka. Dkt. Batilda alibainisha kuwa kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Tanga ina takriban watu 2,615,597. Kutokana na kasi ya chanzo la watu ya asilimia 2.5 kwa mwaka, idadi hiyo inakadiriwa kuwa watu 2,816,711 kwa sasa, ambao wote wana uhakika wa chakula kutokana na msimu wa kilimo wa 2024/2025. "Kulingana na msimu wa msimu uliopita, mkoa umezalisha jumla ya tani 1,814,285 za chakula kikavu kutoka katika hekta 102,076 zilizolimw...

Serikali kutoa mirahaba ya bil 1 kwa wasanii mwakani

  NA MASHAKA MHANDO WIZARA ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kupitia Taasisi ya Hakimiliki nchini (COSOTA), inatarajia kuweka historia mpya kwa kugawa zaidi ya shilingi bilioni moja kama mirabaha kwa wasanii wa kampuni mbalimbali nchini ifikapo Januari 23, 2026. Hatua hiyo inakuja baada ya imani ya kimkakati kati ya Naibu Waziri wa sekta hiyo, Mhe. Hamis Mwinjuma (MwanaFA), na uongozi wa COSOTA, yaliyolenga kujibu kiu ya muda mrefu ya wasanii kuhusu malipo ya haki zao. Akizungumza katika mahojiano maalum, MwanaFA alisema kuwa Serikali imejipanga kufanya ugawaji huo kuwa tukio kubwa na kihistoria kutokana na kiwango kikubwa cha fedha kilichopokea. "Kama msanii kama Naibu Waziri, nilipokea maswali mengi kutoka kwa wasanii wenzangu wakitaka kujua hatma ya mirabaha yao. Nimefanya (discussion) nzuri na COSOTA na tumekubaliana kuwa Januari 23 mwakani, tunakwenda kutoa zaidi ya shilingi bilioni moja na ushee. Himekuwa ni kiwango kikubwa ambacho hakijawahi kutokea nchini," alis...

Dkt. Mwigulu Kukagua Miradi ya Maendeleo Mkoani Lindi

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 19, 2025 amewasili kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara akiwa njiani kuelekea mkoani Lindi kwa ajili ya Ziara ya Kikazi. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu leo anategemea kukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa pamoja na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Madaraja na Ukarabati wa barabara Kuu ya Marendego-Nangurukuru-Lindi-Mingoyo.

Bilioni 11.3 kuzalisha Vitambulisho vya Watoto

Na Mwandishi Wetu Serikali iko katika  Maandalizi ya Usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka 18 ili kutoa namba ya utambulisho ya kipekee ambayo itatolewa tangu mtu anapozaliwa hadi mwisho wa maisha yake ikiwa ni Utekelezaji wa Maelekezo ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyotoa tarehe 10 Agosti,2023. Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene wakati wa ziara ya ukaguzi wa uzalishaji wa vitambulisho katika Kituo cha Kuchakata Taarifa  cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA)  ambapo amaetaja kiasi cha Shilingi Bilioni 11.3 kutengwa kwa ajili ya zoezi  huku wilaya za majaribio zikiwa ni Kilolo, Kusini Unguja na Rungwe ambapo pia ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kufika sehemu walizojiandikisha kuchukua vitambulisho vyao. ‘Jamii namba itakayotambua watoto ndio jambo kubwa ambalo linakuja sasa na itaondoa malalamiko mbalimbali kwani mtu atakua anatambulika kuanzia pale anapozaliwa lak...