Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Uyovu Wamkubali Dkt. Samia, Kumpigia Kura Nyingi Oktoba 29

📌 *Dkt. Biteko kuifanya Uyovu kuwa kitovu cha biashara Bukombe* Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukombe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Doto Mashaka Biteko amesema kuwa mgombe Urais kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameiwezesha Kata ya Uyovu kimaendeleo hivyo wananchi hao hawana budi kumpigia kura nyingi Oktoba 29  mwaka huu. Dkt. Biteko amesema hayo Septemba 17, 2025 wakati wa mkutano wa kampeni katika Kata ya Uyovu wilayani Bukombe mkoani Geita ikiwa ni sehemu Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu. “ Hakuna siku ambayo nilimuomba maendeleo Dkt. Samia kwa ajili ya watu wa Uyovu na Geita akatunyima, ametupa fedha za ujenzi wa barabara nyingi ikiwemo ya kutoka Ushirombo hadi Katoro hata juzi tulimuomba barabara ya Geita kwenda Nzela hadi Sengerema kwa kiwango cha lami yote haya atatusaidia huyu ni mama ni msikivu,” amesema Dkt. Biteko. Ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa Dkt. Samia chini ya CCM kati...

Kongole Takukuru Kuikumbusha Jamii Kukataa Rushwa Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Na: Dkt. Reubeni Lumbagala, Tanga Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Oktoba 29, 2025 ni siku ambayo Taifa letu litafanya Uchaguzi Mkuu ili kuchagua viongozi katika nafasi za urais, ubunge na udiwani. Agosti 28, 2025, kampeni zilizinduliwa rasmi ambapo wagombea walianza kunadi Ilani za vyama vyao na sera zao kwa ujumla katika kipindi cha miaka mitano ijayo 2025-2030 ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo. Rushwa ni moja ya tatizo kubwa hasa kipindi hiki cha uchaguzi kwani baadhi ya wagombea wasio na maadili hutoa rushwa ili kushawishi wapigakura wawapigie kura kuwachagua katika nafasi mbalimbali za uongozi. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) haijalala, ipo macho kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya mapambano dhidi ya rushwa kwa kutumia njia mbalimbali za utoaji elimu ili kuhakikisha nchi yetu inapata viongozi bora wasiotokana na rushwa. Sanjari na hilo, Takukuru imedhamiria kuwachukulia hatua kali wale wote watakaobainika n...

Tutalinda Kwa Bidii Kubwa Tunu za Muungano Wetu -Dkt Samia

 17 Septemba 2025- Kusini Unguja Mgombea wa Urais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan Leo ameendelea na kampeni zake kuinadi Ilani ya CCM Makunduchi, Zanzibar, Katika mkutano wake Dkt. Samia alielezea kuhusu kulinda tunu kuu, muhimu na msingi wa Muungano, Amani na utulivu ili tufikie malengo makubwa kama Taifa. Muungano wetu wa Tanzania ni hazina kubwa na ya kipekee barani Afrika. Ni daraja linalotuunganisha kutoka Visiwani hadi Bara, likitufanya tuwe taifa lenye mshikamano, upendo na ushirikiano wa kweli. Tuwalinde na kuuenzi Muungano huu kwa vitendo, kwani ni urithi wa vizazi vilivyopita na ni dhamana ya vizazi vijavyo.

Kutana na Maajabu ya Mchanga Unaooshwa Tanga

☑️ Watumika kwenye ujenzi wa miradi mikubwa kama Bandari ya Tanga, Bomba la Mafuta EACOP 📍 Tanga, Tanzania Sekta ya Madini nchini inaendelea kushuhudia mageuzi ya kuongeza thamani madini yakiwemo ya ujenzi kama mchanga na kufungua fursa nyingine mpya kwa wachimbaji wadogo wa mchanga kupitia teknolojia bunifu za usindikaji.  Katika mkoa wa Tanga, Kampuni ya Muwa Trading Tanzania Limited imewekeza kwenye Kiwanda cha kuosha na kusafisha mchanga kwa maji ili kuondoa udongo na uchafu mwingine kama mizizi, hatua ambayo imebadilisha kabisa mtazamo wa thamani ya rasilimali hiyo kwa miaka mingi. Kwa mkoa wa Tanga, unaojulikana kwa utajiri wa madini ya viwandani na ujenzi, mchanga safi unaopatikana baada ya kuoshwa sasa ni malighafi yenye thamani kubwa kwa viwanda vya saruji, miradi ya kimkakati ya Serikali ikiwemo Bandari ya Tanga na ujenzi wa Bomba la Mafuta la EACOP katika Kata ya Chongeleani.  Teknolojia hiyo pia inaelezwa kutoa fursa kwa wachimbaji wadogo na wawekezaji kuongeza ma...

Gavana wa Kisiwa cha Moheli aalika Wawekezaji toka Tanzania

Gavana wa Kisiwa cha Moheli nchini  Comoro,Mheshimiwa Chamina Ben Mohamed ametoa wito kwa wawekezaji wa sekta ya Utalii nchini Tanzania kutembelea kisiwa hicho kutathmini fursa katika eneo hilo ikiwemo ujenzi na uendeshaji wa hoteli na pia kuendesha kampuni za kuongoza watalii. Mheshimiwa Chamina ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Comoro,Saidi Yakubu ambaye yupo kisiwani humo kwa ziara ya kujitambulisha kwa wadau mbali mbali. “Kisiwa cha Moheli kina fukwe nzuri kujenga hoteli na kina vivutio zaidi vya Utalii kuliko kisiwa chochote kingine hapa Comoro na natambua Tanzania ina wadau wengi wa kushirikiana nasi,tunawakaribisha” alisema Gavana Chamine. Kwa upande wake,Balozi Yakubu alimueleza Gavana huyo kuwa Sekta ya Utalii ni miongoni mwa sekta zilizopiga hatua kubwa nchini Tanzania na atafikisha ujumbe huo kwa wadau husika. Aidha,Balozi Yakubu alipongeza pia juhudi za Serikali Kuu ya Comoro na Serikali ya Kisiwa hicho katika kuboresha miundombinu ya usa...

Pigeni Kura Oktoba 29, Mtudai Maendeleo - Dkt. Biteko

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukombe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Doto Mashaka Biteko amewaeleza wananchi wa Bukombe kuwa maendeleo yaliyopatikana jimboni humo yametokana na upendo wa Rais Samia Suluhu Hassan kwao, hivyo wajitokeze kuwapigia kura wagombea wa CCM ifikapo Oktoba 29 mwaka huu ili waendelee kupata maendeleo. Dkt. Biteko amesema hayo Septemba 16, 2025 katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Runzewe Magharibi wilayani Bukombe mkoani Geita ikiwa ni sehemu Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu. Amesema katika kipindi cha miaka mitano ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan chini ya CCM imefanya kazi kubwa ya kuleta miradi ya maendeleo katika Kata hiyo ambayo miundombinu yake imefunguka zikiwemo ujenzi wa barabara, shule, miradi ya maji. Ameutaja  mradi wa Msasa ambao upo mbioni kupanuliwa ili kuhudumia wananchi wengi zaidi. Ameongeza kuwa katika kipindi hicho wamejenga Ofisi mpya ya Halmashauri...