Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Joshua Murumbe ateuliwa kuwa katibu wa,NEC,UCHUMI na fedha CCM

  Hongera sana Ndg. Joshua Chacha Mirumbe kwa kuaminiwa kuwa Katibu wa NEC Uchumi na Fedha wa Chama Cha Mapinduzi

Watatu wa Familia Moja Mbaroni kwa Mauaji ya Baba Mzazi

 Na Ada Ouko GMTV Musoma. JESHI la polisi mkoa wa Mara linawashikilia watu watatu wa familia moja wakazi wa Mtaa Nyabisare Kata ya Bweri kwa tuhuma za mauaji ya Chacha Mwita (55) ambaye alikuwa ni Baba mzazi wa familia hiyo. Kamanda wa polisi mkoa wa Mara amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Agosti 20,2025 na kuwataja watuhumiwa hao kuwa ni Matiku Chacha Manyengo(22), Mwajuma Chacha Nyamsiwa(45) na Manyengo Chacha Manyengo(26) ambapo walikuwa wakifanya shughuli za kilimo. "Agosti 14,2025 Jeshi la polisi mkoa wa Mara lilipokea taarifa kutoka kwa watuhumiwa hao kuhusu kupotea kwa ndugu yao ambaye ni mume wa Mwajuma pia ni Baba mzazi wa watumiwa Matiku na Manyengo, mara baada ya kupata taarifa hiyo Jeshi la polisi mkoa wa Mara lilianza uchanguzi mara moja" Amesema Lutumo. Katika uchunguzi wa tukio hilo Kamanda Lutumo amesema jeshi hilo lilibaini kuwa Julai 29, 2025 saa tatu asubuhi nyumbani kwa marehemu kulitokea ugomvi baina ya marehemu na mke wake, ambapo watoto wa marehemu w...

Jeshi La Magereza Mkoa Wa Mara Laadhimisha Miaka 64 Kwa Kutoa Huduma Kwa Jamii

 Na Ada Ouko GMTV, Musoma. JESHI la Magereza mkoa wa Mara limeadhimisha miaka 64 ya kuasisiwa kwake kwa kushiriki matendo ya huruma kwa jamii, ikiwa ni pamoja na kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kata ya Kwangwa Manispaa ya Musoma. Kamishina msaidizi wa jeshi hilo, Mkuu wa magereza mkoani humo Hospitius Mendi amesema maadhimisho hayo yamezinduliwa leo Agosti 23,2025 nchini kote na kwamba kilele chake kitafanyika Agosti 26,2025 lengo likiwa ni kutoa elimu kwa jamii juu ya shughuli zingine zinazotolewa na jeshi hilo tofauti na kurekebisha maadili kwa wafungwa. " Tunaenda maeneo kama hayo ili jamii iweze kutambua kuwa jeshi la Magereza hatufanyi tu kazi ya kuwachunga wafungwa pekee yake lakini ni pamoja na kushirikiana na jamii kwenye maendeleo na kuhifadhi mazingira katika hali ya usafi na usalama wa wananchi kwa ujumla" alisema Mendi. Amesema kauli mbiu ya maadhimisho hayo inasema"Ushirikiano wa Jeshi la M...

Raie Samia aongoza Halmashuri Kuu ya kuteua jina moja la wagombea wa CCM

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani akiongoza kikao cha Halmashuri Kuu ya CCM Taifa, ambacho kinafanya uteuzi wa mwisho wa majina ya Wanachama waliyoomba nafasi za Ubunge na Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Jimbo na Viti Maalum leo Jumamosi Agosti 23,2025 mkoani Dodoma.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Atembelea Mradi wa Gesi Madimba

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari akiongozana na  baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ametembelea  Kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Madimba na Vitalu vya gesi asilia vilivyoko Msimbati Mkoani Mtwara,  tarehe 21 Agosti, 2025. Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema kuwa ziara hiyo itawaongezea maarifa Watumishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Upekuzi wa Mikataba na utoaji wa Ushauri kwenye Miradi mikubwa ukiwemo mradi huo mkubwa wa gesi na mafuta.  *"Tunapoona mradi huu maana yake ni kwamba kuna mikataba ilitangulia mwanzo mikataba ambayo iliandikwa na kupekuliwa vizuri na vihatarishi vyote vikawekwa vizuri na maslahi ya Taifa yakazingatiwa vizuri."* Alisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali  Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema kuwa ziara hiyo ni sehemu ya mafunzo kwa Wataalamu wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mafunzo ambayo yatawasaidia kuwaongezea uwezo katika masuala ya kiufundi kuhusiana n...

Sagini Aendelea Kuboresha Miundombinu Shule ya Awali na Msingi Mwalimu Nyerere

Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini ameendelea kuboresha miundombinu ya Shule ya Awali na Msingi Mwalimu Nyerere iliyopo Kijiji cha Butiama ili kuepukana na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo watumishi na wanafunzi ikiwemo wizi wa vifaa vya kujifunzia. Akizungumza katika Mahafali ya Tano ya Darasa la Saba yaliyofanyika Agosti 22, mwaka huu Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini, Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Emmanuel Mayeji aliyemwakilisha Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini amesema kuwa Mhe Sagini alianza kutatua kero hiyo mapema na sasa ni zoezi la ukamilishaji wa ujenzi wa uzio wa shule. "Mhe. Sagini amewaahidi kwamba atakuwa nanyi bega kwa bega katika kukuza elimu wilayani  Butiama kwani ni maelekezo ya Chama cha Mapinduzi kupitia Ilani ya Uchaguzi wa mwaka 2020 – 2025 iliyolenga kuimarisha ubora wa elimu katika ngazi zote kwa kuzingatia falsafa ya kujitegemea yenye kuendana na mazingira ya nchi yetu," amesema May...