Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Uhuru Kenyata;Nitaunga Mkono Raila Odinga Kuwania Urais ikiwa ataachana na Rais Ruto

  CHAMA cha Jubilee kinachoongozwa na Rais Mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta kimetangaza kuwa kiko tayari kumuunga mkono Kinara wa ODM Raila Odinga kuwania urais 2027 kikisema kuwa bado kinamtambua kama Kiongozi wa Muungano wa Azimio. Naibu Mwenyekiti wa Jubilee David Murathe, amesema kuwa Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, jana aliwaambia kuwa yupo tayari kumuunga Raila mnamo 2027 mradi tu asambaratishe uhusiano wake na utawala wa sasa. Bw Kenyatta jana aliongoza mkutano wa Kamati Kuu ya Jubilee kwenye makao makuu ya chama hicho, kikao kilichofanyika baada ya mrengo wake kushinda kesi ya mzozo wa uongozi wa Jubilee mahakamani. “Bado tunamtambua Raila kama kiongozi wa Azimio. Na kama muungano tunaamua mwelekeo wetu, hata hivyo nakuambia tuko na Tinga (Raila) hadi hali iwe vingine. Raila ndiye kiongozi wetu na Uhuru mwenyekiti wetu,” akasema Bw Murathe. “Watu pia wanaweza kuamua tuunde muungano mpya na tuwashirikishe viongozi wengine zaidi,” akaongeza. Chama cha Jubilee kinaonekana kimeshaa...

Umoja na Mshikamano ni Silaha ya Mtangamano Imara wa Sadc

Umoja na mshikamano imeelezwa kuwa ni silaha pekee ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ya kuimarisha mtangamano imara na wenye nguvu, utakaowezesha kufikia malengo yaliyowekwa na jumuiya hiyo. Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kikao cha Maafisa Waandamizi wa SADC ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Biashara za Kimataifa wa Zimbabwe, Balozi Albert Chimbindi alipokuwa anasoma hotuba ya ufunguzi ya kikao hicho jijini Antananarivo Agosti 06, 2025. Katika kikao hicho ambacho ujumbe wa Tanzania unaongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban imeshuhudiwa Zimbabwe kupitia Balozi Chimbindi ikikabidhi uenyekiti wa kikao hicho kwa Madagascar ambapo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Eric S. Ratsimbazafy alipokea na kuahidi kuendeleza yale yote mazuri yaliyoanzishwa na mtangulizi wake. Balozi Chimbindi alisema katika kipindi cha uenyekiti wake, mtangamano wa SADC umeendelea kuimarika na mafanikio makubwa yamepa...

Mchengerwa: Miaka 10 ya mapinduzi ya fikra, naomba ridhaa tuijenge Rufiji ya ndoto yetu

Na John Jayros  Mbunge anayetetea jimbo la Rufiji Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema katika kipindi chote amekuwa mtumishi wa watu, mwanamapinduzi wa kweli anayejali maendeleo ya wananchi hivyo amewaomba wajumbe wampe ridhaa ya kuwaongoza ili kuendelea kuleta maendeleo. Kauli hiyo ameitoa leo kwenye mkutano wa kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kesho kwenye kura za maoni kuwa mgombea wa jimbo hilo kwa mara ya tatu mfulizo. Mkutano huo umefanyika Ikwiriri na uliohudhuriwa na maelfu ya wajumbe na wananchi waliokuja kusikuliza sera za watia nia wanne wa jimbo hilo ikiwa ni pamoja na Mhe. Mchengerwa anayetetea jimbo lake. Amesema katika kipindi chake cha miaka 10 cha mapinduzi ya fikra na mageuzi makubwa ya maendeleo jimboni humo kumekuwa na mabadiliko kwenye kila sekta. "Ndugu zangu katika safari hii sote tumejionea mapinduzi na mafanikio yaliyopatikana hivyo nawaombeni kwa kasi hii hii nipeni imani ili tuendelee kufanya maendeleo ya kweli ya jimbo letu". Amesisitiza Mhe. Mchengerwa  A...

Maendeleo ya Elimu ni Mkombozi wa Taifa Lolote Duniani-Majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa maendeleo katika sekta ya elimu ndio mkombozi na mafanikio ya Taifa lolote duniani. Amesema kwa kutambua hilo, uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan uliamua kuwekeza katika sekta hiyo ili kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata elimu bora katika ngazi zote. Amesema hayo wakati alipozungumza na wanafunzi na walimu wa shule ya sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia iliyopo Ruangwa mkoani Lindi, wakati wa hafla ya kuwapongeza wanafunzi wa kidato cha sita waliofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa iliyofanyika mwaka 2025. “Mliopo shuleni na mnaokuja, tambueni kuwa tuna maeneo muhimu ya kuwaelimisha, mtapata elimu iliyobora na imara itakayowapa maarufa na ujuzi ili muweze kukabiliana na changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi” Amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita imefanya maboresho ya mitaala kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya kiuchumi yaliyopo duniani ikiwemo mahitaji makubwa ya ajira kwa vijana. “Mabadiliko haya yameifanya mitaa...

Mtasingwa Aibuka Kidedea Kura za Maoni Ccm Jimbo la Bukoba Mjini

  BUKOBA MJINI Mhandisi Johnston Mtasingwa mgombea ubunge wa jimbo la Bukoba Mjini mkoani Kagera kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) ameibuka kidedea katika kura za maoni kwa kupata kura 1,408 huku wenzake wanne walioshiriki uchaguzi huo wakipata kura 1,550. Akitangaza matokeo hayo Katibu wa CCM Wilaya la Bukoba Mjini, Shaban Mdoe ametangaza matokeo hayo ambapo amewataja wengine waliogombea kuwa ni Alex Denis aliyepata kura 804 , Almasoud Kalumuna kura 640 Jamila Hassan kura 66 na Koku Rutha kura 44 Amesema kuwa, wapiga kura waliojiandikisha walikuwa 3,033 waliojitokeza kupiga kura ni 2,978 kura zilizoharibika ni 20 na kura halali zilikuwa ni 2,958.

Mkurugenzi TAMISEMI awataka wananchi kusafisha mitaro ya maji kuzunguka maeneo yao

#Aipongeza TARURA kuendelea kufungua barabara vijijini #Wananchi wa Kimangaro-Mwika Kaskazini wafurahia ushirikiano wa TARURA Dodoma Mkurugenzi wa Idara ya Tawala za Mikoa kutoka OR-TAMISEMI Bi. Beatrice Kimoleta amewataka wananchi kujenga tabia ya kufanya usafi wa mitaro  ya  maji kuzunguka maeneo yao. Bi. Kilemeta ameyasema hayo alipotembelea banda la Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwenye Maonesho ya NaneNane Kitaifa kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma. Amesema kwamba wapo baadhi ya wananchi hawasafishi mitaro ya maji kwenye barabara zinazopita kwenye nyumba zao na hivyo maeneo yao kuwa machafu wakati wote. “TARURA endeleeni kutoa elimu kwa wananchi wasafishe mitaro inayopita kwenye nyumba zao,ipo mitaa unakuta kuna barabara nzuri za lami lakini kuna nyasi nyingi na wengine wana magenge mbele ila uchafu wote wanatupa kwenye mitaro hiyo na hawasafishi”. Ameongeza kusema kwamba wananchi wakijenga utamaduni wa kusafisha na kulinda miundombinu ya barabara...