Mhandisi Johnston Mtasingwa mgombea ubunge wa jimbo la Bukoba Mjini mkoani Kagera kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) ameibuka kidedea katika kura za maoni kwa kupata kura 1,408 huku wenzake wanne walioshiriki uchaguzi huo wakipata kura 1,550.
Akitangaza matokeo hayo Katibu wa CCM Wilaya la Bukoba Mjini, Shaban Mdoe ametangaza matokeo hayo ambapo amewataja wengine waliogombea kuwa ni Alex Denis aliyepata kura 804 , Almasoud Kalumuna kura 640 Jamila Hassan kura 66 na Koku Rutha kura 44
Amesema kuwa, wapiga kura waliojiandikisha walikuwa 3,033 waliojitokeza kupiga kura ni 2,978 kura zilizoharibika ni 20 na kura halali zilikuwa ni 2,958.