Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Waziri Mkuu Atembelea Kiwanda Cha Dawa na Zana za Kilimo Nchini Belarus

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa, leo tarehe 22 Julai 2025, ameendelea na ziara yake rasmi nchini Belarus kwa kutembelea maeneo muhimu ya uzalishaji na ushirikiano wa kimkakati.  Akiwa katika mji wa Minsk, Mheshimiwa Majaliwa alitembelea kiwanda cha Belmedpreparaty, ambacho ni maarufu kwa utengenezaji wa dawa za binadamu. Aidha, Waziri Mkuu pia alitembelea kiwanda cha Minsk Tractor Plant, ambacho kinajihusisha na utengenezaji wa matrekta na mitambo ya kisasa ya zana za kilimo. Ujumbe wa Tanzania ulijionea teknolojia ya hali ya juu inayotumika katika uzalishaji wa vifaa hivyo. Wakati wa ziara hiyo, pamoja na viongozi wengine, Waziri Mkuu aliambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Cosato Chumi. Mheshimiwa Majaliwa pia aliweka shada la maua katika mnara wa mashujaa wa Jamhuri ya Beralus. Kwa ujumla, ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Tanzania kuimarisha mahusiano ya kimataifa kwa manufaa ya wananchi, hasa katika sekta muhimu za m...

Rais Samia Atoa Bilioni Nne Ujenzi Kiwanda Cha Kuzalisha Nishati Mbadala

📌Kiwanda kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa nishati safi nchini 📌REA kugharamia ununuzi wa mtambo wa STAMICO 📌Stamico yapania kusambaza Nishati Safi ya Rafiki Briquettes kila kona Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) leo tarehe 22 Julai, 2025 wamesaini mkataba wenye lengo la kujenga kiwanda kipya cha kuzalisha nishati mbadala (Mkaa mbadala wa Rafiki Briquettes) mkoani Geita ambapo mkataba huo una thamani ya shilingi bilioni 4.5. Katika hafla iliyofanyika katika Ofisi ndogo ya REA, Jijini, Dar es Salaam, REA itatoa jumla ya shilingi bilioni tatu na STAMICO itatoa shilingi bilioni 1.5; kwa mchanganuo huo, REA itagharamia ununuzi wa mtambo wakati STAMICO italipia upatikanaji wa kiwanja, ujenzi wa jengo la kiwanda na gharama za ufungaji wa mitambo.  Mkataba huo umesainiwa na Mhandisi, Hassan Saidy, Mkurugenzi Mkuu wa REA pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt. Venance Mwasse. Mkataba huo utaifanya STAMICO kuwa na ...

EMEDO yaeleza Juhudi zake kwenye kusimamia miradi ya inayogusa Jamii

  Mwandishi wetu ;TANGA Shirika la Environmental Management and  Economic Development Organization  (EMEDO)limefafanua utekelezaji wa miradi mbalimbali yenye tija katika jamii kwenye kikao cha pamoja Kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja Mashirika yasiyo ya Kiserikali  kinachofanyika Jijini Tanga. Afisa Mawasiliano wa EMEDO Peter Kimisha akishiriki  hatua ya awali ya  kueleza mategemeo ya Shirika kwenye mkutano huo  aliweka bayana kuwa EMEDO inakiona kikao hicho kuwa ni fursa ya kueleza mbele ya wadau wengine utekelezaji wa kazi zake Kwa Mwaka 2025 - 2026 pamoja na kutengeneza mahusiano mkakati na wadau wengine. Peter Pia alieleza umuhimu wa kikao hicho ni kuuelewa vyema muongozo wa mashirikiano baina ya Sekta ya Uvuvi na Asasi za Kiraia zinazofanya kazi kwenye eneo la uvuvi. Naye Bwana Edwin Soko, Mjumbe wa Bodi wa EMEDO alitoa wasilisho zuri lililoeleza shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Shirika la EMEDO kwenye eneo la uchumi na mazingira ndan...

EMEDO Yaeleza Juhudi Zake Kwenye Kusimamia Miradi inayogusa Jamii

Mwandishi wetu ;TANGA Shirika la Environmental Management and  Economic Development Organization  (EMEDO)limefafanua utekelezaji wa miradi mbalimbali yenye tija katika jamii kwenye kikao cha pamoja Kati ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja Mashirika yasiyo ya Kiserikali  kinachofanyika Jijini Tanga. Afisa Mawasiliano wa EMEDO Peter Kimisha akishiriki  hatua ya awali ya  kueleza mategemeo ya Shirika kwenye mkutano huo  aliweka bayana kuwa EMEDO inakiona kikao hicho kuwa ni fursa ya kueleza mbele ya wadau wengine utekelezaji wa kazi zake Kwa Mwaka 2025 - 2026 pamoja na kutengeneza mahusiano mkakati na wadau wengine. Peter Pia alieleza umuhimu wa kikao hicho ni kuuelewa vyema muongozo wa mashirikiano baina ya Sekta ya Uvuvi na Asasi za Kiraia zinazofanya kazi kwenye eneo la uvuvi. Naye Bwana Edwin Soko, Mjumbe wa Bodi wa EMEDO alitoa wasilisho zuri lililoeleza shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Shirika la EMEDO kwenye eneo la uchumi na mazingira ndani ya se...

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awasili Nchini Belarus Kwa Ziara ya Kikazi

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) amewasili jijini Minsk, Belarus kwa ziara ya kikazi ya siku nne kuanzia tarehe 21 hadi 24 Julai 2024.  Alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa nchi hiyo, Mhe. Waziri Mkuu alipokewa na Naibu Waziri Mkuu wa Belarus, Mhe. Viktor Karankevich na viongozi wengine waandamizi wa nchi zote mbili akiwemo Waziri wa Uwekezaji, Zanzibar, Mhe. Sharif Ali Sharif; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi na Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Mhe. Fredrick Kibuta. Ziara hiyo ambayo  ni ya kwanza kwa kiongozi wa ngazi ya juu nchini Tanzania kuifanya nchini Belarus, inalenga kuendeleza mkakati wa Serikali zote mbili wa kuimarisha uhusiano wa uwili hususan katika sekta za kimkakati ikiwemo kilimo, elimu, afya, utalii, uwekezaji, biashara na uhaulishaji wa teknolojia. Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Waziri Mkuu atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Waziri Mkuu wa Belarus, Mhe. ...

Kambi ya Kutengeneza Mishipa ya Damu, Upandikizaji Figo Yaanza Rasmi Muhimbili Mloganzila

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imeanza kambi maalum ya kutengeneza mishipa ya kuchuja damu sambamba na kupandikiza figo kwa wagonjwa wenye changamoto za figo ambayo itahitimishwa rasmi Julai 23, 2025. Kambi hiyo inafanywa na wataalam wa Muhimbili Mloganzila kwa kushirikiana na jopo la wataalam kutoka Korea Kusini linalo ongozwa na Prof. Park Kwan Tae ambaye ni Daktari Bingwa Bobezi wa Upasuaji chini ya uaratibu wa Taasisi ya Africa Future Foundation (AFF) ya nchini Korea Kusini. Upandikizaji wa figo unafanyika kwa kuvuna figo kutoka kwa mchangiaji kwa kutumia matundu madogo (Laparascopic Hand Assisted Donor Nephroctomy) utaalam ambao kwa hapa nchini unapatikana Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila pekee. Aidha,wataalam mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wanajengewa uwezo wa kutoa huduma hizo katika maeneo yao ili kuwapunguzia wananchi usumbufu wa kwenda mbali na maeneo yao kufuata huduma hizo. Hadi kuhitimishwa kwa kambi hiyo wananchi takribani 60 watanufaika na huduma ...