Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Tatu bora wa CCM " UBUNGE " kujulikana Julai 19 mwaka 2025

 

Global Education Link yawausia wanafunzi wanaokwenda kusoma nje ya nchi

Na Mwandishi Wetu WAZAZI ambao watoto wao wanakwenda kusoma nje ya nchi kwa mwaka wa masomo wa 2025/2026 wametakiwa kufuatilia kwa karibu mwenendo wa watoto wao kitaaluma na tabia. Wito huo ulitolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Elimu Nje ya Nchi, Global Education Link (GEL),  Abdulmalik Mollel alipokutana na wazazi na wanafunzi hao siku ya Jumapili kwenye ofisi za GEL jijini Dar es Salaam ambapo wazazi na wanafunzi hao walipewa taratibu  za mambo ya kuzingatia kabla, wakati na baada ya kufika nchi wanazokwenda. Katika mkutano huo, ambao ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka vyuo vikuu mbalimbali duniani, wanafunzi wengi walikabidhiwa viza zao tayari kwa ajili ya safari ya kuelekea vyuoni, huku wazazi wakipata fursa ya kuzungumza ana kwa ana na baadhi ya wawakilishi wa vyuo hivyo. Akizungumza wakati wa mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel, alisema wazazi wanalipolipa ada wasidhani kwamba wamemaliza jukumu lao na badala yaake bado wa...

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Wa Nchi Za Falme za Kiarabu Afanya Ziara Nchini Tanzania

 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa nchi za Falme za Kiarabu, Luteni Jenerali Eisa Saif Mohamed Bin Ablan Almazrouei amefanya ziara ya kikazi nchini Tanzania leo tarehe 14 Julai 2025. Jenerali Almazrouei alipokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda. Mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Upanga Jijini Dar es Salaam, Luteni Jenerali Almazrouei alipokea salamu ya heshima na kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yake.  Wakati wa mazungumzo yake mafupi na ujumbe huo toka Falme za Kiarabu ofisini kwake Upanga, Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda alieleza umuhimu wa ushirikiano wa Kijeshi uliopo baina ya Mataifa haya mawili kuwa unaendelea kudumishwa. Jenerali Mkunda amesema JWTZ linajivunia, ushirikiano uliopo katika kukabiliana na matishio ya kiusalama kama vile ugaidi na usafirishaji haramu wa binadamu katika nchi mbili hizi. Aidh...

Balozi Nchimbi Aongoza Kikao Cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu Taifa Dodoma

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akiongoza kikao cha kawaida cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, leo Julai 14, 2025 katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM (White House) mkoani Dodoma. Kikao hicho, kinachotarajiwa kuendelea hadi Julai 16, kimeitishwa kufuatia kukamilika kwa zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania uteuzi wa nafasi za uwakilishi katika vyombo vya dola. Nafasi hizo zinahusisha ubunge wa majimbo, ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, viti maalum vya ubunge na Baraza la Wawakilishi, pamoja na udiwani wa kata na viti maalum.

Waziri Mkuu Majaliwa Akabidhi Tuzo ya Umahiri Kwa Mkuu Wa Kitengo Cha Mawasiliano Wizara ya Nishati

*📌Ni kufuatia Umahiri wa masuala ya Mawasiliano kwenye Maonesho ya Osaka Expo 2025*  ðŸ“Œ *Ampongeza kwa kuwa Kiongozi wa mfano wakati wa Mkutano wa Biashara na Uwekezaji na Utalii Osaka Expo 2025* Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa leo tarehe 13 Julai, 2025 amemkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Nishati, Bi Neema Chalila Mbuja tuzo ya umahiri kufuatia mchango wake  alioutoa wakati wa Maonesho ya Dunia ya Biashara ya Osaka nchini Japan kwa upande wa Mawasiliano na kuitangaza nchi. Mhe Majaliwa amempongeza Bi. Mbuja wakati wa kilele cha  Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba 2025. Sambamba na hilo Mhe Majaliwa amempongeza Bi. Mbuja kwa kuwa muongozaji wa shughuli na kuwa mahiri wakati wa Kongamano la Kimataifa la Biashara, Uwekezaji na Utalii kwenye Maonesho ya Osaka Expo 2025. Kwa upande wake Bi. Mbuja amemshukuru Mhe. Majaliwa kwa kukabidhi tuzo hiyo iliyotolew...

Hospitali ya Benjamin Mkapa nchini Tanzania kutoa matibabu ya kibingwa nchini Burundi