Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba imemhukumu Baraka Anyongwe hadi Kufa Kwa Kosa la Kumuua Mama Mzazi

Angela Sebastian; Bukoba Mkazi wa kitongoji kijiji cha Mwanga wilaya ya Biharamlo mkoani Kagera Emmanuel Barakanfitye maarufu kama rais (52) amehukumiwa kunyongwa hadi kufa katika mahakama kuu kanda ya Bukoba baada ya kupatikana na kosa la mauaji ya mama yake mzazi aliyejulikana kwa jina la Mariana Matabaro. Mawakili upande wa Jamhuri katika kesi hiyo walikuwa ni Matrida Assey pamoja na Gloria Lugeye. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Bukoba,Wakili wa Serikali Matrida Assey amesema kuwa, hukumu hiyo imetolewa Mei 30,2025 baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa pande wa Jamhuri pasipo kuacha shaka lolote hivyo kumtia hatiani na kumuhukumu kifungo cha kunyongwa hadi kufa. Amesema tukio hilo la mauaji ya Mariana Matabaro (75) lilitokea Mei 13, 2020 ambapo aliuawa na mtoto wake wa kumzaa Emmanuel akishirikiana na mshitakiwa wa pili Jackson Emmanuel (21) ambaye alikuwa mjukuu wa marehemu ambapo kijana huyo wakati wa tukio alikuwa na miaka (16). Assey akizumg...

Dc Chikoka Afungua Kongamano la Madini na Kuhimiza Ufatiliaji wa Elimu

Na Shomari Binda-Musoma  MKUU wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amefungua kongamano la maonyesho ya ya madini mkoa wa Mara huku akihimiza wachimbaji kufatilia elimu itakayotolewa. Maonyesho ya madini mkoa wa Mara yameingia katika siku ya pili hii leo juni 4,2025 huku kongamano hilo linalowashirikisha wachimbaji,wauzaji na wachenjuaji likifanyika kwenye ukumbi wa Mwembeni Complex Akifungua kongamano hilo Chikoka amesema anaamini palipo na mafanikio kunatikana na kuwa na elimu kama inavyokwenda kutolewa kupitia kongamano hilo. Amesema washiriki wanapaswa kufatilia kila mada itayotolewa ili kupata uelèwa wa kila jambo litakalofundishwa katika mnyororo mzima wa sekta ya madini Chikoka amesema kongamano hilo lina umuhimu wa pekee katika kujifunza na kufikia lengo la serikali ya mkoa wa Mara kufikia uchimbaji uchimbaji wenye tija. Amesema amepata taarifa juu ya mada 5 zinawasilishwa siku ya leo na kuwa na majadilino na kutaka kusikiĺzwa na kujadiliana kwa pamoja. " Nami leo nimetenga mud...

Waziri Mchengerwa Awafunda Walimu

  Na John Mapepele  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa rai kwa walimu nchini kuwa wazalendo na kuzingatia weledi ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi.  Mhe. Mchengerwa ametoa rai hiyo kwenye mkutano wa walimu na wadau wa elimu  wa Wilaya ya Rufiji uliofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari ya Wasichana Bibi Titi Mohamed, ambapo yeye mwenyewe pia alitunukiwa tuzo ya heshima ya kutambua mchango wake katika sekta ya elimu wilayani Rufiji. "Katika hali ya kawaida  Serikali imeboresha mazingira na miundombinu ya sekta ya elimu kilichobaki ni kwa sisi walimu kutanguliza uzalendo ili kuinua kiwango cha elimu katika ngazi zote" . Amesisitiza Mhe. Mchengerwa  Aidha, amesisitiza walimu kutambua wajibu wao na kwamba Serikali haitaweza kusita kuwachukulia hatua za kinidhamu  Walimu na Maafisa Elimu ambao watakuwa wazembe katika utekelezaji wa majukumu yao. Katika taarifa ya Wilaya ya Rufiji kwa Mhe. Waziri, iliyoandaliwa na...

Dkt. Nindi: Tume ya Umwagiliaji ipanue wigo wa huduma nchini

📍 NIRC Dodoma.  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo anayeshughulikia Ushirika na Umwagiliaji, Dkt. Stephen Nindi, ameitaka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kutanua wigo wa kazi zake kwa kuwafikia wadau jumuishi wa sekta nyingine lengo likiwa ni  kuhakikisha kilimo cha umwagiliaji kinakuwa na tija katika maendeleo ya jamii.   Nindi amesema hayo alipotembelea banda la Tume ya Taifa ya Umwagiliaji viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dodoma katika maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani. Dkt. Nindi amesema kuwa pamoja na kazi nzuri inayofanywa na Tume, ni vyema taasisi hiyo muhimu katika sekta ya kilimo ikaendelea kutanua wigo ili kuwafikia wadau wengine, mbali na wakulima wa mazao pekee. “Wakulima wa umwagiliaji si tu wanajikita kwenye kilimo, bali pia wanajihusisha na uvuvi, ufugaji na matumizi ya maji ya nyumbani. Ni muhimu kuweka mikakati inayozingatia uhitaji huu mtambuka ili kuongeza tija na matumizi endelevu ya rasilimali," amesema Dkt. Nindi.   Katika kuende...

Dkt.Kijaji Awaonya Wananchi Uharibifu Wa Mazingira na Athari za Mifuko ya Plastiki

Na Mwandishi wetu Jovina Massano. Watanzania wameonywa kuachana na matumizi ya mifuko ya plastiki kwani athari zake ni kubwa kwa afya ya binadamu na viumbe hai pamoja na mazingira kwa ujumla. Wito huo umetolewa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alipotembelea mabanda ya maonesho wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Juni 2, 2025 yanayoendelea kwenye Viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma. Mhe. Dkt. Kijaji alisema kuwa mifuko ya plastiki isipodhibitiwa ikitupwa ovyo na kuingia kwenye vyanzo vya maji vikiwemo bahari na maziwa ina athari kubwa kwa samaki na mazalia yake. “Sote tutatambue mifuko hii si salama kwa maisha yetu pamoja na mifugo na samaki, kwa mfano inapoingia baharini samaki wenyewe wakimeza mifuko hii ya plastiki haiwezi kumeng’enywa na mwisho wake hufa". Aidha Waziri Dkt. Kijaji ametoa wito kwa wafugaji wote nchini kuzingatia ufugaji ulio endelevu usioweza kuharibu mazingira ikiwemo kukata miti ovyo kwa ajili ya m...

Balozi Nchimbi Msibani kwa Mzee Mongella

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akisaini kitabu cha maombolezo na kumpatia pole, Mama Gertrude Ibengwe Mongella, familia yake na waombolezaji wengine, kwa msiba wa Mzee Silvin Ibengwe Emmanuel Mongella, ambaye ni mwenza wa Mama Mongella, leo Jumanne, tarehe 3 Juni 2025, eneo la Makongo juu, jijini Dar Es Salaam.  Marehemu Mzee Mongella (85), ambaye pia ni baba mzazi wa John Mongella, Naibu Katibu Mkuu wa CCM (bara), alifariki tarehe 31 Mei 2025, na mazishi yake yamepangwa kufanyika huko Mwanza, tarehe 7 Juni 2025.