Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Azania Bank Yashinda Tuzo Ya Ubora Kidijitali Afrika Mashariki 2o25

Benki ya Azania imeibuka mshindi katika tuzo za Africa Bank 4.0 Awards 2025 zilizotolewa jijini Nairobi, Kenya hivi karibuni ikiwa ni Benki inayoongoza kwa mageuzi ya huduma za kidijitali Afrika Mashariki kwa mwaka 2025.  Tuzo za Africa Bank Awards hutolewa na taasisi ya kimataifa ya BII Finance, zina lengo la kutambua mchango wa taasisi za fedha katika kuleta mageuzi ya huduma za Kidijitali na ubunifu unaoweza kuwarahisishia huduma watumiaji. Kwa Azania Bank, tuzo hii ni muendelezo wa mabadiliko makubwa ya huduma za Kidijitali yanayofanywa na Benki hiyo siku hadi siku. Baadhi ya Watanzania wameipongeza benki hiyo kwa ushindi huo na kusema inastahili kupata tuzo hiyo kutokana na huduma bora zinazotolewa na benki hiyo.

Balozi Nchimbi Aboresha Taarifa Zake Kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akiwa kwenye kituo cha uandikishaji wapiga kura kilichopo katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kilimani, Mtaa wa Kilimani, jijini Dodoma, kwa ajili ya kuboresha taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, leo tarehe 20 Mei, 2025.

Nyihita Agro Consultancy Yafikisha Elimu Ya Kilimo Biashara Rorya

  Na Shomari Binda-Rorya  KAMPUNI ya Nyihita Agro Consultancy kwa kushirikiana na Serikali wamekuja na utoaji elimu kuhusu kilimo biashara kwa wanafunzi na wananchi wilayani Rorya. Elimu hiyo ni kuwafanya wakulima kulima kilimo cha uhakika na kuwawezesha kunufaika kiuchumi na kuweza kusaidia familia ikiwa ni pamoja na masuala ya elimu. Akizungumza na wazazi na wanafunzi kwenye shule ya sekondari Mika iliyopo Wilaya ya Rorya jana mei 19,2025 baada ya kutoa elimu ya upandaji kwa wanafunzi,mkurugenzi wa kampuni ya Nyihita Sunflower Wilfred Nyihita amesema wazazi wasichukulie elimu hiyo kwa wanafunzi kama adhabu. Amesema serikali na kampuni yake imekuja na mpango wa kuwainua wananchi kiuchumi kupitia kilimo na kama wanafunzi watashika elimu hiyo na kuwafikishia wazazi namna ya kupanda mbegu mashambani kila familia itainuka kiuchumi. Nyihita amesema kilimo kwa sasa kimekuwa mkombozi na serikali kupitia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ipo began kwa bega na wakulima hivyo Rorya lazima i...

Majaliwa: Watanzania Tuendelee Kumtunza Mdudu Nyuki

_▪️Asema lengo ni kuwa na Taifa lenye uhakika wa chakula na uchumi imara_ _▪️Azindua mpango wa kuendeleza sekta ya ufugaji nyuki kwa Tanzania iliyo bora_   WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuendelea kumtunza na kumuhifadhi nyuki ili kuwa na Taifa lenye uhakika wa chakula na uchumi ulio imara kwa kuwa takribani asilimia 80 ya mimea ya chakula inayozalishwa duniani huchavushwa na nyuki. Pia, Waziri Mkuu amezindua mpango kabambe utakaoleta mageuzi makubwa ya sekta ya ufugaji nyuki nchini, unaojulikana kama Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Ufugaji Nyuki kwa Tanzania Iliyo Bora (Achia Shoka, Kamata Mzinga).  Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Mei 20, 2025) wakati akifunga Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani, ambayo kitaifa yamefanyika katika Kiwanja cha Chinangali jijini Dodoma. Ametoa wito kwa wadau wote wa masuala ya nyuki kushirikiana na Serikali kuwezesha utekelezaji wa mpango huo. “Serikali inatumia maadhimisho kuhimiza, kuelimisha na kuhamasisha Watanzani...

Vyombo Vya Ulinzi na Usalama Msitoe Nafasi Kwa Watovu wa Adabu-Rais Samia

  Rais Samia: “Tusiwe shamba la bibi” - aonya wanaharakati wa nchi jirani kutoingilia masuala ya Tanzania Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametoa onyo kali kwa wanaharakati kutoka nchi jirani kuacha kuingilia masuala ya ndani ya Tanzania, akisisitiza kuwa taifa hilo haliwezi kuwa “shamba la bibi” ambapo kila mtu anaingia na kufanya apendavyo. Akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa toleo jipya la Sera ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001 (Toleo la 2024), Rais Samia amesema kuna mwenendo unaoibuka wa baadhi ya wanaharakati kuvuka mipaka na kuingilia masuala ya ndani ya nchi, hali ambayo haiwezi kuvumiliwa. “Tusuiwe shamba la bibi kwamba kila mtu anaweza kuja na kusema anachokitaka… Tumeanza kuona mtitiriko au mwenendo wa wanaharakati ndani ya region (kanda) yetu hii, kuanza kuvamia na kuingilia mambo yetu huku,” alisema Rais Samia. Kauli hiyo inakuja siku moja baada ya wakili mashuhuri wa Kenya na aliyewahi kuwa Waziri wa Sheria, Martha Karua, pamoja na Jaji Mkuu wa zaman...

Rais Dkt. Samia Kufungua Daraja La Jp Magufuli (Kigongo - Busisi) Juni 19, 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya ufunguzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi) lenye urefu wa kilometa 3 na barabara zake unganishi zenye urefu wa kilometa 1.66 utakaofanyika tarehe 19 Juni, mwaka huu. Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo tarehe 19 Mei, 2025 wakati alipokagua daraja hilo ambalo limekamilika kujengwa na litakuwa daraja refu zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. "Jitayarisheni kwa wingi kumpokea kiongozi wetu mkuu atakapokuja kulifungua daraja hili Juni 19, 2025 ", amesema Waziri Mkuu Majaliwa. Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega ameeleza kuwa Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa Daraja hilo linalopita juu ya maji kwa kutumia fedha za ndani ikiwa ni jambo la kihistoria kwa nchi yetu. Ameongeza kuwa zaidi ya shilingi bilioni 700 zimetumika katika ujenzi wa daraja hilo linalounganisha mji wa Kigo...