Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Gachagua azindua chama cha DCP huku genge likijaribu kutibua hafla

 ALIYEKUWA Naibu Rais Rigathi Gachagua hatimaye amezindua chama chake kipya, Democracy for the Citizens Party (DCP), kama hatua ya kujiandaa kumenyena kisiasa na aliyekuwa mkubwa wake, Rais William Ruto wa chama cha United Democratic Alliance (UDA). Nembo ya chama kipya ni sikio linalosikiliza, na kauli mbiu yake ni “Skiza Wakenya”, ikiwa na rangi za kijani kibichi yenye mwangaza, nyekundu ya kutu, na nyeupe. Bw Gachagua alijiteua kuwa kiongozi wa chama na akawatangaza kaimu maafisa watakaosimamia chama hicho kipya. “Kama Kiongozi wa Chama cha Democracy for the Citizens Party, naahidi kwamba nitasikiliza watu wa Jamhuri ya Kenya na kutimiza matamanio yao,” alisema Bw Gachagua. Uchambuzi wa majina yaliyotangazwa unaonyesha kuwa wengi wao ni wanasiasa walioshindwa katika uchaguzi mkuu uliopita. Wengine ni watu wasiojulikana sana. Baadhi ya washirika wa Bw Gachagua walichaguliwa kwa tiketi ya UDA na wako hatarini kufukuzwa kwa kujihusishwa waziwazi na chama kipya, jambo lililowafanya...

Dkt. Biteko Ateta na Spika Wa Bunge La Morocco

📌 Tanzania, Morocco wakubaliana kuimarisha ushirikiano Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe Dkt. Doto Biteko Mei 15, 2025 ametembelea Bunge la Morocco ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi nchini humo. Akiwa Bungeni hapo, Dkt. Biteko amefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la nchi hiyo Mhe. Rachid Talbi El Alami na Naibu Spika Mhe. Lahcen Haddad katika ofisi za Bunge hilo zilizoko jijini Rabat nchini Morocco. Pamoja na mambo mengine, wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizo mbili hususan katika Sekta ya Nishati, Kilimo, Viwanda na Biashara. 

Diwani Merysiana Atoa Ujumbe Siku ya Familia Duniani

Na Shomari Binda-Musoma  WAZAZI kwenye familia wametakiwa kutatua migogoro ya kifamilia pale inapojitokeza ili kujiepusha kutengana na watoto kukosa malezi bora. Hayo yamesemwa na diwani wa viti maalum manispaa ya Musoma Meryciana Masasi leo mei 15,2025 alipozungumza na GMTV ikiwa ni siku ya familia duniani. Amesema wimbi la watoto wa mitaani linazalishwa na mambo mengi ikiwa ni pamoja na migogoro inayojitokeza kwenye familia. Diwani huyo amesema iwapo migogoro inapojitokeza na kushindwa kusuruhishwa upelekea wazazi kutengana na watoto kukosa malezi hivyo kukimbilia mitaani. Amesema watoto kukosa malezi ya pande mbili huwa kunatokea changamoto ya kimalezi na kushauri kuwepo na utatuzi wa migogoro ili kuepusha tatizo hilo. " Kupitia siku hii ya familia duniani nitoe ushauri kwa wazazi kuwa na utaratibu wa utatuzi wa migogoro ili tuwalee watoto wetu kwa pamoja na kujenga familia. " Watoto hatupendi waangaike mitaani na wanakuwa wanapata tabu na hii kwa asilimia kubwa inatokana ...

Misa-tan, Wan Ifra Na Thrdc Waendesha Mjadala Uendelevu Vyombo Vya Habari Katika Mawanda Ya Uchumi Unaobadilika

Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA TAN) kwa kushirikiana na Umoja wa Wachapishaji wa Magazeti Ulimwenguni (WAN-IFRA) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeendesha mjadala kuhusu uendelevu wa vyombo vya Habari katika mawanda ya uchumi unaobadilika uliowashirikisha wadau mbalimbali wa Habari nchini. Baadhi ya wadau hao ni wamiliki wa vyombo vya Habari, Wahariri wa Vyombo vya Habari, Wahadhiri wa Vyuo vya Uandishi wa Habari na Viongozi wa Taasisi za Habari. Katika mjadala huo, wadau hao wa sekta ya habari walijadili mambo mbalimbali ikiwemo sheria na kanuni za uchaguzi. Kwa upande wake Mwenyekiti wa MISA Tan Edwin Soko amechangia mjadala huo na kusema, kunahitajika jitihada za pamoja kati ya Taasisi za usimamizi wa Vyombo vya habari nchini, Wamiliki wa Vyombo vya habari na waandishi wa habari kukaa pamoja kwenye kujadili uendelevu na uhimilivu wa Vyombo vya habari kwani kufanya hivyo kutasaidia kuwa na mikakati ya pamoja ya namn...

Misa Tan Yamlilia Charles Hillary

Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA Tan), imetoa salamu za pole kufuatia kifo cha mwanahabari mkongwe Charles Hillary, ikisema itaendelea kukumbuka mchango wake mkubwa katika sekta ya habari hapa nchini. Mwenyekiti wa MISA Tan, Edwin Soko, amesema kuwa marehemu Hillary alikuwa na mchango mkubwa sana katika kukuza taaluma ya habari na kutetea uhuru wa vyombo vya habari. “Tumempoteza mtu muhimu sana katika tasnia ya habari. Charles Hillary alikuwa mfano wa kuigwa kwa wanahabari wengi kutokana na weledi, ujasiri na kujitolea kwake kwa maslahi ya taaluma,” alisema Soko. MISA Tan imeeleza kuwa itaendelea kuenzi ujasiri wa marehemu kwenye kuipambania sekta ya habari na pia inatoa pole Kwa familia na watanzania wote

Mke wa Rais wa Finland Suzanne Innes-Stubb atembelea Makumbusho ya Taifa la Tanzania

Mke wa Rais wa Finland Suzanne Innes-Stubb atembelea Makumbusho ya Taifa la Tanzania Ujio wa ziara hiyo umefanyika leo tarehe 14/05/2025 Makumbusho ya Taifa la Tanzania katika kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni kilichopo Posta, Dar es salaam. Ziara hii ni utangulizi wa ziara ya kesho tarehe 15/05/2025 ambapo Makumbusho ya Taifa inatarajia kumpokea Rais wa Jamhuri ya Finland, Alexander Stubb, aliyewasili jijini Dar es Salaam, Tanzania kwa ziara rasmi ya siku tatu kuanzia Mei 14 hadi 16, 2025. Akiwa kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Mke wa Rais wa Finland Bi. Suzanne Innes-Stubb alipokelewa kwa ngoma za asili kisha wenyeji wake Dkt. Hassan Abbasi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Dkt. Noel Lwoga, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania walimkaribisha. Akiongea baada ya kumpitisha maeneo mbalimbali na kujionea mikusanyo na historia ya Tanzania iliyohifadhiwa kituoni hapo Dkt. Lwoga amesema ni mafanikio makubwa ya Serikali ya awamu ya sita kati...