Skip to main content

Posts

@marato_tv

@marato_tv
#sauti_ya_jamii

Mhandisi Mativila aridhishwa Utekelezaji wa Miradi ya Barabara ya Mtili-Ifwagi na Sawala-Iyegeya

Iringa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila ametembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa barabara za Mtili–Ifwagi na Sawala-Iyegeya, ambapo ameonesha kuridhishwa na miradi hiyo. Barabara hizo zinazojengwa na TARURA kwa lengo la kurahisisha usafirishaji wa mazao ya chai, misitu, mbogamboga na mazao mengine kufika sokoni kwa  wakati. Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi hiyo ili kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana huku akitoa wito kwa wakandarasi kuendelea kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia muda uliopangwa.  Wananchi nao wametoa pongezi kwa serikali kwa kuwaletea maendeleo yanayoonekana na yanayogusa maisha yao ya kila siku. Barabara hizo zinatarajiwa kurahisisha usafiri, kukuza biashara na kuongeza upatikanaji wa huduma muhimu kama afya na elimu katika maeneo ya vijijini.

Rais Samia Awafikia Watanzania Zaidi ya Milioni Mbili Na Kutatua Migogoro Zaidi ya Elfu Tano

Jumla ya wananchi 2,774,495 wakiwemo wanawake 1,390,535 na wanaume 1,381,960 wamepatiwa huduma za Msaada wa Kisheria tangu kuzinduliwa kwa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia kwa upande wa Tanzania Bara mwezi Machi 2023. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Jumanne Sagini wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia  mkoani Kusini Unguja uliofanyika katika viwanja vya Mtende-Azimio leo 10/05/2025 ambapo mgeni rasmi alikua Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi. Mhe. Sagini ameongeza kuwa migogoro 5,704 imetatutliwa kati ya migogoro 23,399 ya muda mrefu iliyoibuka huku migogoro 18,987 ikiwa katika hatua mbalimbali za utatuzi na utekelezaji wa kampeni tayari umefikia Mikoa 25, halmashauri 180 na vijiji/mitaa 8702 ya Tanzania bara huku mkoa uliosalia wa Dar es Salaam ukitarajiwa kukamilika mwezi Juni 2025. Aidha Mhe.Sagini amesema kuwa wananchi waliofikiwa na kampeni hii wamepata huduma mbalimbali i...

Katibu Mkuu wa Ccm Balozi Emmanuel Nchimbi Ashiriki Kuaga Mwili wa Mzee Cleopa Msuya

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akitoa salaam na heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa Hayati Mzee Cleopa David Msuya, Makamu wa Kwanza na Waziri Mkuu Mstaafu. Shughuli hiyo iliyoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, baada ya ibada, iliyofanyika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar Es Salaam, leo Jumapili, tarehe 11 Mei 2025.

Wanafunzi TUSIIME kufundishwa program za kompyuta kuanzia msingi hadi sekondari

Na Mwandishi Wetu KATIKA jitihada za kuendana na mtaala mpya wa elimu uliozinduliwa hivi karibuni na Serikali, unaojumuisha Mahili 11 yanayolenga kuendeleza ujuzi na stadi kwa wanafunzi, shule za Tusiime zimechagua program za Kompyuta kama kipaumbele chao. “Tukiwa na dira ya kuandaa wanafunzi kwa maisha ya kesho yanayotawaliwa na teknolojia, hususan katika zama hizi za akili mnemba Artificial Intelligence (AI), shule zetu za  Tusiime kuanzia shule ya awali, msingi na sekondari mpaka kidato cha sita zimeanza rasmi utekelezaji wa somo la Introduction to Complete Programming kwa wanafunzi wa ngazi mbalimbali,” amesema leo Mkurugenzi wa shule hizo, Dk Albert Katagira. Alisema lengo la kuanza kufundisha program za kompyuta ni kuhakikisha kuwa wakifika kidato cha sita, kila mwanafunzi wa Tusiime awe na ujuzi mpana wa kujua program mbalimbaali za kompyuta. Dk Katagira alisema mafunzo hayo yatamwezesha mwanafunzi kujiajiri kupitia utengenezaji wa programu rahisi, kuunda vikundi vya program...

"Amani iwe nanyi nyote,” Ujumbe wa kwanza wa Papa Leo XIV

AMANI iwe nanyi! Ndugu wapendwa, hii ndio ilikuwa salamu ya kwanza ya Kristo aliyefufuka, mchungaji mwema aliyeutoa uhai wake kwa watu Mungu. Mimi pia ningependa salamu hii ya amani iingie mioyoni mwenu, ifikie familia zenu na watu wote, popote walipo; na mataifa yote, na dunia yote: Amani iwe nanyi. Hii ndiyo amani ya Kristo aliyefufuka, amani isiyo na silaha, ya unyenyekevu na ya kudumu. Inatoka kwa Mungu. Mungu ambaye anatupenda sote, bila mipaka wala masharti. Tuweke masikioni mwetu sauti dhaifu lakini daima ya ujasiri ya Papa Francis, aliyebariki Roma – Papa aliyebariki Roma na dunia siku ile ya asubuhi ya Pasaka. Niruhusuni kuendeleza baraka hiyo hiyo. Mungu anatupenda, sisi sote, na uovu hautashinda. Sote tuko mikononi mwa Mungu. Bila hofu, tukiwa pamoja, mkono kwa mkono na Mungu na sisi kwa sisi, tutaendelea mbele. Sisi ni wanafunzi wa Kristo, Kristo yuko mbele yetu, na dunia inahitaji mwanga wake. Ubinadamu unamhitaji kama daraja la kumfikia Mungu na upendo wake. Ninyi hutusai...

Mnec Joyce Ryoba Mang'o Amshukuru Rais Dkt.Samia Kwa Msaada wa Kisheria

Na Shomari Binda-GMTV MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Joyce Mang'o amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa msaada wake wa kisheria kwa watanzania. Shukrani hizo amezitoa jana mei 10,2025 visiwani Zanzibar aliposhiriki tukio la uzinduzi wa kampeni ya Mama Samia Legal Aid ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Dkt.Hussen Ally Mwinyi. Akizungumza baada ya uzinduzi huo amesema kampeni hiyo imekuwa msaada mkubwa tangu ilipozinduliwa nchi nzima. Amesema amepita maeneo mengi na kusikia sauti za wanufaika wa msaada huo wa kisheria hasa wanawake wakimshukuru Rais Dkt.Samia. MNec huyo  amesema wapo wanawake waliotatuliwa matatizo yao papo kwa papo na wale wenye kesi Mahakamani wamepatiwa mawakili wa kuweza kuwasaidia. " Tunamshukuru sana mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa maono yake na kuanzisha kampeni hii ya msaada wa kisheria. " Kila nilipohudhuria uzinduzi wa kampeni nimeona namna watanzania wavyotoa shukrani zao kwa namna walivyosaidiwa kwa kupata m...