Na Shomari Binda-Bunda MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amezungumzia namna alivyofanya kazk na marehemu Mhandisi Boniphace Gissima Nyamo-Hanga wakati akiwa Waziri wa Nishati na Madini. Akitoa salamu za rambirambi leo aprili 16,2025 wakati wa maziko yake yaliyofanyika eneo la Migungani wilayani Bunda amesema Taifa limepoteza kijana ambaye mchango wake bado ulikuwa ukihitajika. Amesema afanya kazi na Mhandisi Nyamo-Hanga mwaka 2012 na alikuwa msikivu na kupokea maelekezo hasa kwenye suala la kasi ya kupeleka umeme vijijini na kupata mafanikio yanayotajwa leo kwenye suala la umeme. Muhongo amesema kila mara alikuwa akijitisha vikao kuitisha vikao vya kuuliza namna bora ya kupeleka umeme vijijini ili wananchi wapate nishati hiyo. Mbunge huyo amesema kazi nzuri iliyofanyika kwenye eneo hilo ilipelekea dunia kutambua kazi nzuri iliyofanywa na kutaka kutambua njia gani iliyotumika maka kufanikiwa. Amesema kupunguza gharama za umeme na kuweka gharama nafuu ya um...
Marato tv - Sauti ya Jamii